Sunday, 26 February 2012

FAIDA YA TAQWA (Ucha Mungu)

Anasema Allaah سبحانه وتعالى

((... وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا )) (( وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لاَ يَحْتَسِبُ ..))

((Na atakayekuwa na taqwa (kumcha Allaah) Humtengezea njia ya kutokea)) ((Na Humruzuku pasinakutegemea)) [At-Twalaaq: 2-3]

Hizo ni kauli za Allaah سبحانه وتعالى katika Kitabu Chake Qur-aan Tukufu, ambayo ni Uongofu kamili wa mwanaadamu.
Kitabu kisichokuwa na shaka wala kufikiwa na ubatilifu mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikma Ahimidawaye.

Taqwa ni wasiya wa watu wa mwanzo na wa mwisho, na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliwausia Maswahaba wake wapenzi :

عن أبي ذَرٍّ جُنْدُب بِن جُنَادَة، وأبي عبد الرحمن مُعَاذ بِن جَبَلٍ رضي الله عنهما، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((اتق الله حيثما كنت، وأَتْبِعِ السَّيئةَ الحسنةَ تَمْحُها، وخالقِ الناسَ بخُلُقٍ حسنٍ)). رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ .

Kutoka kwa Abu Dharr Jundub Ibn Junaada na Abu Abdur Rahmaan Mu'adh Ibn Jabal رضي الله عنهما ambao wamemnukuu Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: ((Mche Allaah popote pale ulipo, na fuatisha kitendo kibaya kwa kitendo kizuri kitafuta (kitendo kibaya), na ishi na watu kwa uzuri))

Na Taqwa haihitajii kuhakikishwa kuwa mahali fulani au wakati fulani, bali taqwa ya hakika ni pale mtu anapokua yuko peke yake, akajiepusha na yaliyo haraam japokuwa hakuna mtu anayemuona.
Na ndipo aliposema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuwa 'Taqwa iko hapa' akiashiria kwenye kifua chake palipo na moyo na kusema mara tatu.

Thursday, 23 February 2012

Vipi Tunaweza Kufaidika Na wakati?
1. Kukumbuka kifo na misukosuko yake.
2. Kujizowesha kuthamini wakati na umuhimu wake katika kutekeleza ahadi.
3. Kukumbuka jambo gani muhimu la kufanya ili upate radhi za Allah.
4. Kuihesabu nafsi yako kuwa umefanya lipi la kumridhisha Allah.
5. Kukumbuka mwisho wa kila jambo baya na adhabu itakayomkabili kila mwenye kutumia wakati kwa kufanya maovu.
6. Kukumbuka wasia na mafundisho ya Mtume s.a.w juu ya kufanya matendo mema na malipo yake.
7. Kuandaa muongozo au ratiba ya kuendeleza mambo yako ya kila siku ambayo ni msingi katika maisha.
8. Kujiepusha na tabia ya kusahau.
9. Kushiriki katika mambo muhimu ya jamii na kutoa kila unachoweza kutoa kwa ajili ya kuisaidia jamii, kwani utaja ulizwa siku ya masiku kuwa umetanguliza kitu gani katika vitu alivyokujaalia Allah juu ya jamii uliyokuwa unakaa.
10. Kusoma vitabu mbali m bali vya mafundisho ya dini kujua kuwa Mtume s.a.w pamoja na msahaba na watu wema waliyokuja baada ya Mtume s.a.w na masahaba zake kujua walikuwa wanafaidika vipi na wakati.
11. kuwa na mazoeya ya kusoma kitabu kitakatifu cha Allah wakati ambao upo katika kusubiria kitu au usafiri (kituoni) au ndani ya chombo cha usafiri ukiwa katika safari ndefu, ili mradi usikubali kupitwa na neema hii ya wakati.
12. Tufahamu kuwa wenzetu wanafanikisha vipi mambo yao kwa kuchunga wakati, hasa hasa makafiri, kwani hujulikana kuwa ni watu wenye kuzingatia sana wakati kuliko hata tulivyo sisi ambao Mungu ametuletea muongozo wa mitume na vitabu vitukufu vyenye kila m uogozo wa maisha yetu, lakini kwa masikitiko makubwa sisi ndio watu wa mwanzo katika kupoteza neema ya wakati na kusahau thamani yake.

Allaah tumuombe atujaaliye tuwe watu wa kuthamini wakati.

Wednesday, 1 February 2012

SOMO LA TAREKH (DARASA LA KWANZA

MBINU ZA KUFUNDISHIA
• Mwalimu ataje majina ya Mitume 25 na kuwataka wanafunzi wamfuatishe.
• Aorodheshe majina 25 kwenye ubao na kuwaamuru wanafunzi kuandika.
• Asisitize kwa wanafunzi kuwa Mitume wote wamekuja kufundisha Uislamu.

VIFAA VYA KUTUMIA
Vitabu vya Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) na vitabu vya visa mbali mbali za Mitume ya Allah.

LENGO.
Afahamu kuwa Mitume wote wamekuja kufundisha Uislamu.
Mtume wa Allah Muhammad(S.A.W.) kuwa ni Mtume ni Mtume wa mwisho.
KWA NINI UISLAMU UMEHARAMISHA WANAUME KUVAA DHAHABU NA HARIRI?

Leo ulimwenguni kote kutokana na kile kinachojulikana kama wimbi la kwenda na wakati, uhuru na haki ya mtu kufanya/kuishi atakavyo; si jambo la kushangaza wala kustaajabisha kuwaona vijana wa kiume wakiwa wamejipamba kwa kuvaa mikufu, pete na hata hereni za dhahabu.
Hili leo si geni tena bali ni jambo la kawaida na fakhari hata katika miji ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, ambako asilimia kubwa ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu kwa miongo ya miaka.
Uvaaji huu wa dhahabu kwa vijana wa kiume umeingizwa pande zetu hizi za Afrika ya Mashariki na vijana waliotoka huku kwenda nchi za Ulaya kutafuta ajira hasa ya ubaharia. Hawa waliporejea wakiwa wameuiga utamaduni huo wa kigeni na kuwaathiri vijana wengine, limbukeni wenye kuiga kila kiingiacho mjini.
Utamaduni huu wa vijana wa kiume kujipamba kwa kuvaa dhahabu unakwenda kinyume na utamaduni wa mila ya Kiislamu.
Mwenyezi Mungu amemuumba mwanamume na Mwanamke na kumpa kila mmoja maumbile na tabia zinazotofautiana na mwenzake. Ikiwa hili linaashiria kitu, basi si kingine bali ni kutofautiana pia katika nafasi na majukumu ya kila mmoja wao. Nadharia inaonyesha kuwa tabia na maumbile ya mwanaume ni ukakamavu na ugumu, wakati ambapo tabia na maumbile ya kike ni ulaini na ulegevu.
Uislamu unamtaka mwanaume alelekee katika mazingira yaliyo mbali na udhaifu,unyonge na anasa zinazoweza kunlegeza ili aweze kuwa imara na mwenye nguvu katika kupambana na harakati za maisha ya kila siku, ambapo sehemu kubwa ya jukumu hilo amebebeshwa yeye na sheria .
Sasa kwa kuzingatia kuwa madini ya dhahabu na hariri ni vitu vya anasa ambavyo humfanya mvaaji aonekane amependeza machoni mwake yeye mwenyewe kwanza na machoni mwa wengine na natija yake ni kuvaana na maumbile ya kupendeza ambayo ni ulaini na ulegevu.
Pengine kwa njia moja au nyingine hii ndio inaweza kuwa hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri kwa wanaume kwa kuwa inakubaliana na tabia na maumbile yao. Hebu tujaribu kuwa wakweli, tuwatie katika mizani ya haki na uadilifu wanaume wenye kuvaa dhahabu na wasiovaa dhahabu, tutagundua nini? Bila ya shaka mtakubaliana na mimi kuwa ipo tofauti ya dhahiri baina yao, wavaao dhahabu watakuwa wameathirika na tabia na maumbile ya kike.
Taathira hii utaiona katika mwendo wao, uzungumzaji wao, uvaaji wao na wakati mwingine huiga hasa tabia za kike kama vile kusuka nywele na kutumia vipodozi.
Ni kweli usiopingika kwamba kujua hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri kwa wanaume, hii ni elimu isiyo na manufaa na ni ujinga usiodhuru.
Usiulize hekima kwa kuwa kumeshurutishwa katika kuulizia hekima ya amri au makatazo, awe huyo muamrishaji/mkatazaji analingana sawa na kufanana na huyo muamrishaji/mkatazwaji na hapa ni suala la Mungu Muumba Muamrishaji na mwanadamu kiumbe muamrishwa. Kwa mantiki hii mwanadamu hana budi kuikubali na kuipokea amri kwa kuwa Mola wake ameamrisha/amekataza,kisha baada ya kutekeleza aliloamrishwa ndipo anaweza kutafuata kujua hekima/falsafa ya amri ile.
Lakini kule kujua hekima/falsafa iliyomo katika amri au katazoisiwe ni sharti ambalo kwanza ni lazima litimizwe kabla ya kuamrika au kukatazika. Muislamu wa kweli anaambiwa na Mola wake:
“HAIWI KWA MWANAUME ALIYEAMINI WALA KWA MWANAMKE ALIYEAMINI, ALLAH NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAURI,WAWE NA HIARI KATIKA SHAURI LAO. NA MWENYE KAMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, HAKIKA AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI (kabisa) [33:36]
Kuharamishwa uvaaji wa dhahabu kwa wanaume kumethibiti katika hadithi nyingi sahihi zilizopokelewa kutika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu –Rehema na Amani zimshukie.

1. Amepokea (riwaya) Imamu Bukhaariy, Muislam na Ahmad kwamba Mtume wa Allah “Amekataza (kuvaa) pete ya dhahabu”.
2. Imepokelewa kutoka kawa Ibn Abbaas-Allah awawiye radhi-kwamba Mtume wa Allah aliiona pete ya dhahabu kidoleni mwa mtu, akamvua na kuitupa (huku) akisema “ Mmoja wenu analikusudia kaa la moto na kulivaa mkononi?” Mtu yule akaambiwa baada ya kwenda zake mtume “ Itwae pete yako unufaike nayo. Akawajibu Wallah hapana, kamwe sitaichukua ikiwa aliyeitupa ni Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie.” Muislam.
3. Na katika jumla ya riwaya zilizopokelewa kwamba Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie amesema : “ Ye yote mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho basi asivae hariri wala dhahabu.” Al-musnad {Musnadul–Imam Ahmad}