FAIDA YA TAQWA (Ucha Mungu)
Anasema Allaah سبحانه وتعالى
((... وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا )) (( وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لاَ يَحْتَسِبُ ..))
((Na atakayekuwa na taqwa (kumcha Allaah) Humtengezea njia ya kutokea)) ((Na Humruzuku pasinakutegemea)) [At-Twalaaq: 2-3]
Hizo ni kauli za Allaah سبحانه وتعالى katika Kitabu Chake Qur-aan Tukufu, ambayo ni Uongofu kamili wa mwanaadamu.
Kitabu kisichokuwa na shaka wala kufikiwa na ubatilifu mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikma Ahimidawaye.
Taqwa ni wasiya wa watu wa mwanzo na wa mwisho, na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliwausia Maswahaba wake wapenzi :
عن أبي ذَرٍّ جُنْدُب بِن جُنَادَة، وأبي عبد الرحمن مُعَاذ بِن جَبَلٍ رضي الله عنهما، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((اتق الله حيثما كنت، وأَتْبِعِ السَّيئةَ الحسنةَ تَمْحُها، وخالقِ الناسَ بخُلُقٍ حسنٍ)). رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ .
Kutoka kwa Abu Dharr Jundub Ibn Junaada na Abu Abdur Rahmaan Mu'adh Ibn Jabal رضي الله عنهما ambao wamemnukuu Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: ((Mche Allaah popote pale ulipo, na fuatisha kitendo kibaya kwa kitendo kizuri kitafuta (kitendo kibaya), na ishi na watu kwa uzuri))
Na Taqwa haihitajii kuhakikishwa kuwa mahali fulani au wakati fulani, bali taqwa ya hakika ni pale mtu anapokua yuko peke yake, akajiepusha na yaliyo haraam japokuwa hakuna mtu anayemuona.
Na ndipo aliposema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuwa 'Taqwa iko hapa' akiashiria kwenye kifua chake palipo na moyo na kusema mara tatu.
No comments:
Post a Comment