Vipi Tunaweza Kufaidika Na wakati?
1. Kukumbuka kifo na misukosuko yake.
2. Kujizowesha kuthamini wakati na umuhimu wake katika kutekeleza ahadi.
3. Kukumbuka jambo gani muhimu la kufanya ili upate radhi za Allah.
4. Kuihesabu nafsi yako kuwa umefanya lipi la kumridhisha Allah.
5. Kukumbuka mwisho wa kila jambo baya na adhabu itakayomkabili kila mwenye kutumia wakati kwa kufanya maovu.
6. Kukumbuka wasia na mafundisho ya Mtume s.a.w juu ya kufanya matendo mema na malipo yake.
7. Kuandaa muongozo au ratiba ya kuendeleza mambo yako ya kila siku ambayo ni msingi katika maisha.
8. Kujiepusha na tabia ya kusahau.
9. Kushiriki katika mambo muhimu ya jamii na kutoa kila unachoweza kutoa kwa ajili ya kuisaidia jamii, kwani utaja ulizwa siku ya masiku kuwa umetanguliza kitu gani katika vitu alivyokujaalia Allah juu ya jamii uliyokuwa unakaa.
10. Kusoma vitabu mbali m bali vya mafundisho ya dini kujua kuwa Mtume s.a.w pamoja na msahaba na watu wema waliyokuja baada ya Mtume s.a.w na masahaba zake kujua walikuwa wanafaidika vipi na wakati.
11. kuwa na mazoeya ya kusoma kitabu kitakatifu cha Allah wakati ambao upo katika kusubiria kitu au usafiri (kituoni) au ndani ya chombo cha usafiri ukiwa katika safari ndefu, ili mradi usikubali kupitwa na neema hii ya wakati.
12. Tufahamu kuwa wenzetu wanafanikisha vipi mambo yao kwa kuchunga wakati, hasa hasa makafiri, kwani hujulikana kuwa ni watu wenye kuzingatia sana wakati kuliko hata tulivyo sisi ambao Mungu ametuletea muongozo wa mitume na vitabu vitukufu vyenye kila m uogozo wa maisha yetu, lakini kwa masikitiko makubwa sisi ndio watu wa mwanzo katika kupoteza neema ya wakati na kusahau thamani yake.
Allaah tumuombe atujaaliye tuwe watu wa kuthamini wakati.
No comments:
Post a Comment