Wednesday 3 October 2012

VITA VYA majimaji “MACHINJIO” YA WAISLAMU


Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge,hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji.

Jambo kubwa la mahala hapo ni Kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na….
walizikwa kwa pomoja.Na kando ya kaburi hilo la pomoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwa mwaka 2007.

Baada ya kusaini kitabu cha wageni,na kulipa ada ya kituo,muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo.

ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa mwislam jambo moja litakustuwa.Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni waislaam .

linaanza jina lake la kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman[Dominic]Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya majimaji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya kikristo na baadae kunyongwa,wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru,wote katika hao walionyongwa walikuwa ni waislam.

Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya Yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake[huyo padri] aliiyaandika hayo majina.

Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo.Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona wakubwa wa kituo hicho.

Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009.nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo,iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya majimaji,haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya majimaji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu,jina la padri,sahihi yake na wadhifa wake katika kanisa katoliki pia vimeondolewa,na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza Muhudumu kulikoni? Akasema……. Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya Tanu na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M.S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na mzungu wa kijerumani.

Binti huyu na na mumewe wa kijerumani walikuja hapa Songea matembezi.

Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha.

Hivyo ndio karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni waislaam,wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano.

Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa pia peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa,unaanza kuona picha za mashujaa wa majimaji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija.

kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani.Chini ya kila picha kuna jina la mwenye picha.Katika picha hizo majina Ukipanda gorofani utaona silaha za kijadi,mikuki,pinde,mishale,ngao,n.k.

Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita.mavazi ya vita ya askari wa majimaji wengi walivaa kanzu za kiislaam na vilemba.

Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika”Rosary”[hili ni jina la kikristo,hasa la kikatoliki,ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba]lakini unapotazama hicho kilichoitwa “Rosary” utaona si Rosary, bali ni Tasbihi hasa ya kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake,33,33,34.maneno yaliyoandikwa kuelezea Rosary hizo ambazo ni Tasbihi ni “Hizi ni Rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.

ukweli ni kwamba hawa askari wa majimaji wengi walikuwa ni waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia Tasbihi hizo kufanya Dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani.

Midhali sisi waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama waislaam,wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka.

Hapo gorofani kuna jingine la kasisimua.kuna makopo au magudulia.

Wameandika kuwa,haya ndio makopo ambayo askari wa majimaji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani[kushika udhu na sio kunawa]pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga na Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za uhakika ziko Jimbo kuu la Wakatoliki,Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.Tulitakiwa tupate kibari cha Askofu mkuu.Hatukukipata.

Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia tulijifunza mambo yafuatayo:-

1.Vita vya majimaji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao.La!!!Vilikuwa ni vita vya waislaam wakipigana na wakristo wa kijerumani waliovamia maeneo asilia ya waislaam kwa lengo la kuuwa uislaam na kusimamisha Kanisa.kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya majimaji ni mazingira ya kiislaam,kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa kijerumani ila katika miji ya waislaam.Kilwa.Bagamoyo.n.k.kwa nini wauliwe maeneo ya waislaam tu?walifuata nini huko?

2.kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya majimaji.Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa kijerumani,wakati ukweli si hivyo.Ukweli ni kwamba vita vya majimaji vilikuwa ni vita baina ya waislaam na wakrito wa kijerumani,waafrika wakristo wa songea walijiunga na wakristo wenzao wa kijerumani dhidi ya waafrika wenzao wa kiislaam.

3.Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao. MWISHO Kuna haja ya wasomi wetu wa kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa Historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri.Taasisi za kiislaam na watu binafsi[matajiri]wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.

Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa kisiwani ,huko nikamkuta mzungu wa kifaransa akiandika historia ya kilwa kisiwani akiitwaThiery,ameweka kambi na majenereta ya umeme,solar power,na makompyuta.kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni Misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale.

Kilwa kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za kiislaam katika mwambao wa Afrika mashariki,ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah.

Tuliposoma kazi ile ya Yule Thiery mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa.sikuwa na la kumfanya.Kizazi cha vijana wa kiislaam hakitopata historia ya kweli ya kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike,na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika uislam wao.

Sunday 26 February 2012

FAIDA YA TAQWA (Ucha Mungu)

Anasema Allaah سبحانه وتعالى

((... وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا )) (( وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لاَ يَحْتَسِبُ ..))

((Na atakayekuwa na taqwa (kumcha Allaah) Humtengezea njia ya kutokea)) ((Na Humruzuku pasinakutegemea)) [At-Twalaaq: 2-3]

Hizo ni kauli za Allaah سبحانه وتعالى katika Kitabu Chake Qur-aan Tukufu, ambayo ni Uongofu kamili wa mwanaadamu.
Kitabu kisichokuwa na shaka wala kufikiwa na ubatilifu mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikma Ahimidawaye.

Taqwa ni wasiya wa watu wa mwanzo na wa mwisho, na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliwausia Maswahaba wake wapenzi :

عن أبي ذَرٍّ جُنْدُب بِن جُنَادَة، وأبي عبد الرحمن مُعَاذ بِن جَبَلٍ رضي الله عنهما، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((اتق الله حيثما كنت، وأَتْبِعِ السَّيئةَ الحسنةَ تَمْحُها، وخالقِ الناسَ بخُلُقٍ حسنٍ)). رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ .

Kutoka kwa Abu Dharr Jundub Ibn Junaada na Abu Abdur Rahmaan Mu'adh Ibn Jabal رضي الله عنهما ambao wamemnukuu Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: ((Mche Allaah popote pale ulipo, na fuatisha kitendo kibaya kwa kitendo kizuri kitafuta (kitendo kibaya), na ishi na watu kwa uzuri))

Na Taqwa haihitajii kuhakikishwa kuwa mahali fulani au wakati fulani, bali taqwa ya hakika ni pale mtu anapokua yuko peke yake, akajiepusha na yaliyo haraam japokuwa hakuna mtu anayemuona.
Na ndipo aliposema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuwa 'Taqwa iko hapa' akiashiria kwenye kifua chake palipo na moyo na kusema mara tatu.

Thursday 23 February 2012

Vipi Tunaweza Kufaidika Na wakati?
1. Kukumbuka kifo na misukosuko yake.
2. Kujizowesha kuthamini wakati na umuhimu wake katika kutekeleza ahadi.
3. Kukumbuka jambo gani muhimu la kufanya ili upate radhi za Allah.
4. Kuihesabu nafsi yako kuwa umefanya lipi la kumridhisha Allah.
5. Kukumbuka mwisho wa kila jambo baya na adhabu itakayomkabili kila mwenye kutumia wakati kwa kufanya maovu.
6. Kukumbuka wasia na mafundisho ya Mtume s.a.w juu ya kufanya matendo mema na malipo yake.
7. Kuandaa muongozo au ratiba ya kuendeleza mambo yako ya kila siku ambayo ni msingi katika maisha.
8. Kujiepusha na tabia ya kusahau.
9. Kushiriki katika mambo muhimu ya jamii na kutoa kila unachoweza kutoa kwa ajili ya kuisaidia jamii, kwani utaja ulizwa siku ya masiku kuwa umetanguliza kitu gani katika vitu alivyokujaalia Allah juu ya jamii uliyokuwa unakaa.
10. Kusoma vitabu mbali m bali vya mafundisho ya dini kujua kuwa Mtume s.a.w pamoja na msahaba na watu wema waliyokuja baada ya Mtume s.a.w na masahaba zake kujua walikuwa wanafaidika vipi na wakati.
11. kuwa na mazoeya ya kusoma kitabu kitakatifu cha Allah wakati ambao upo katika kusubiria kitu au usafiri (kituoni) au ndani ya chombo cha usafiri ukiwa katika safari ndefu, ili mradi usikubali kupitwa na neema hii ya wakati.
12. Tufahamu kuwa wenzetu wanafanikisha vipi mambo yao kwa kuchunga wakati, hasa hasa makafiri, kwani hujulikana kuwa ni watu wenye kuzingatia sana wakati kuliko hata tulivyo sisi ambao Mungu ametuletea muongozo wa mitume na vitabu vitukufu vyenye kila m uogozo wa maisha yetu, lakini kwa masikitiko makubwa sisi ndio watu wa mwanzo katika kupoteza neema ya wakati na kusahau thamani yake.

Allaah tumuombe atujaaliye tuwe watu wa kuthamini wakati.

Wednesday 1 February 2012

SOMO LA TAREKH (DARASA LA KWANZA

MBINU ZA KUFUNDISHIA
• Mwalimu ataje majina ya Mitume 25 na kuwataka wanafunzi wamfuatishe.
• Aorodheshe majina 25 kwenye ubao na kuwaamuru wanafunzi kuandika.
• Asisitize kwa wanafunzi kuwa Mitume wote wamekuja kufundisha Uislamu.

VIFAA VYA KUTUMIA
Vitabu vya Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) na vitabu vya visa mbali mbali za Mitume ya Allah.

LENGO.
Afahamu kuwa Mitume wote wamekuja kufundisha Uislamu.
Mtume wa Allah Muhammad(S.A.W.) kuwa ni Mtume ni Mtume wa mwisho.
KWA NINI UISLAMU UMEHARAMISHA WANAUME KUVAA DHAHABU NA HARIRI?

Leo ulimwenguni kote kutokana na kile kinachojulikana kama wimbi la kwenda na wakati, uhuru na haki ya mtu kufanya/kuishi atakavyo; si jambo la kushangaza wala kustaajabisha kuwaona vijana wa kiume wakiwa wamejipamba kwa kuvaa mikufu, pete na hata hereni za dhahabu.
Hili leo si geni tena bali ni jambo la kawaida na fakhari hata katika miji ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, ambako asilimia kubwa ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu kwa miongo ya miaka.
Uvaaji huu wa dhahabu kwa vijana wa kiume umeingizwa pande zetu hizi za Afrika ya Mashariki na vijana waliotoka huku kwenda nchi za Ulaya kutafuta ajira hasa ya ubaharia. Hawa waliporejea wakiwa wameuiga utamaduni huo wa kigeni na kuwaathiri vijana wengine, limbukeni wenye kuiga kila kiingiacho mjini.
Utamaduni huu wa vijana wa kiume kujipamba kwa kuvaa dhahabu unakwenda kinyume na utamaduni wa mila ya Kiislamu.
Mwenyezi Mungu amemuumba mwanamume na Mwanamke na kumpa kila mmoja maumbile na tabia zinazotofautiana na mwenzake. Ikiwa hili linaashiria kitu, basi si kingine bali ni kutofautiana pia katika nafasi na majukumu ya kila mmoja wao. Nadharia inaonyesha kuwa tabia na maumbile ya mwanaume ni ukakamavu na ugumu, wakati ambapo tabia na maumbile ya kike ni ulaini na ulegevu.
Uislamu unamtaka mwanaume alelekee katika mazingira yaliyo mbali na udhaifu,unyonge na anasa zinazoweza kunlegeza ili aweze kuwa imara na mwenye nguvu katika kupambana na harakati za maisha ya kila siku, ambapo sehemu kubwa ya jukumu hilo amebebeshwa yeye na sheria .
Sasa kwa kuzingatia kuwa madini ya dhahabu na hariri ni vitu vya anasa ambavyo humfanya mvaaji aonekane amependeza machoni mwake yeye mwenyewe kwanza na machoni mwa wengine na natija yake ni kuvaana na maumbile ya kupendeza ambayo ni ulaini na ulegevu.
Pengine kwa njia moja au nyingine hii ndio inaweza kuwa hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri kwa wanaume kwa kuwa inakubaliana na tabia na maumbile yao. Hebu tujaribu kuwa wakweli, tuwatie katika mizani ya haki na uadilifu wanaume wenye kuvaa dhahabu na wasiovaa dhahabu, tutagundua nini? Bila ya shaka mtakubaliana na mimi kuwa ipo tofauti ya dhahiri baina yao, wavaao dhahabu watakuwa wameathirika na tabia na maumbile ya kike.
Taathira hii utaiona katika mwendo wao, uzungumzaji wao, uvaaji wao na wakati mwingine huiga hasa tabia za kike kama vile kusuka nywele na kutumia vipodozi.
Ni kweli usiopingika kwamba kujua hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri kwa wanaume, hii ni elimu isiyo na manufaa na ni ujinga usiodhuru.
Usiulize hekima kwa kuwa kumeshurutishwa katika kuulizia hekima ya amri au makatazo, awe huyo muamrishaji/mkatazaji analingana sawa na kufanana na huyo muamrishaji/mkatazwaji na hapa ni suala la Mungu Muumba Muamrishaji na mwanadamu kiumbe muamrishwa. Kwa mantiki hii mwanadamu hana budi kuikubali na kuipokea amri kwa kuwa Mola wake ameamrisha/amekataza,kisha baada ya kutekeleza aliloamrishwa ndipo anaweza kutafuata kujua hekima/falsafa ya amri ile.
Lakini kule kujua hekima/falsafa iliyomo katika amri au katazoisiwe ni sharti ambalo kwanza ni lazima litimizwe kabla ya kuamrika au kukatazika. Muislamu wa kweli anaambiwa na Mola wake:
“HAIWI KWA MWANAUME ALIYEAMINI WALA KWA MWANAMKE ALIYEAMINI, ALLAH NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAURI,WAWE NA HIARI KATIKA SHAURI LAO. NA MWENYE KAMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, HAKIKA AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI (kabisa) [33:36]
Kuharamishwa uvaaji wa dhahabu kwa wanaume kumethibiti katika hadithi nyingi sahihi zilizopokelewa kutika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu –Rehema na Amani zimshukie.

1. Amepokea (riwaya) Imamu Bukhaariy, Muislam na Ahmad kwamba Mtume wa Allah “Amekataza (kuvaa) pete ya dhahabu”.
2. Imepokelewa kutoka kawa Ibn Abbaas-Allah awawiye radhi-kwamba Mtume wa Allah aliiona pete ya dhahabu kidoleni mwa mtu, akamvua na kuitupa (huku) akisema “ Mmoja wenu analikusudia kaa la moto na kulivaa mkononi?” Mtu yule akaambiwa baada ya kwenda zake mtume “ Itwae pete yako unufaike nayo. Akawajibu Wallah hapana, kamwe sitaichukua ikiwa aliyeitupa ni Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie.” Muislam.
3. Na katika jumla ya riwaya zilizopokelewa kwamba Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie amesema : “ Ye yote mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho basi asivae hariri wala dhahabu.” Al-musnad {Musnadul–Imam Ahmad}

Tuesday 31 January 2012

NAMNA YA KUPANGILIA WAKATI:

Kupangilia wakati ndio njia ya mafanikio. Vitabu vya dini vinahimiza watu wawe na ratiba ya mambo ya ibada na mengineyo. Mtu asiye na ratiba hana mafanikio maishani vyovyote atakavyokuwa.
Kwani kujipangia ratiba ni sawa na methali ya Kiswahili isemayo “Mali bila ya daftari hulika bila habari” wakati ni mali, na mtu asiye na ratiba mara nyingi hupoteza wakati mwingi bila habari! Ukijiwekea ratiba nzuri itakusaidia kutekeleza mambo yako kwa ufanisi. Lengo la kurasa hizi ni kutoa mwongozo juu ya namna ya kujipangia ratiba ya kila siku.

NAMNA YA KUPANGA RATIBA.
1) Kwanza kabisa, fahamu kile unachokihitaji kukitenda kwa siku nzima. Kisha jipe muda maalum wa kukamilisha kila tendo.
2) Jaribu kuweka uwiano mzuri (balanzi) yaani jipe muda wa kutosha kwa ajili ya kazi, mapunziko, kutazama TV, kuongea na marafiki, kupiga soga katika utandawazi, kufanya mazoezi, muda wa ibada, kutembelea ndugu, nk.
3) Kwa muda wa kujifunza, jaribu kuupangia ratiba katika nyakati ambazo unakuwa mchangamfu na hakuna vishawishi kama mechi za soka, michezo ya kuigiza, na kitu chochote upendacho kukifanya kwa wakati huo.
4) Jitahidi utenge muda wa kujifunza takriban kila siku, chagua muda kwa kila siku wa kujifunza sio mbaya kama kutakuwa na mapunziko siku moja au mbili kwa wiki.
5) Kila siku jipe muda huru usio wa kufanya kitu chochote, ndani ya muda huo waweza kufanya lolote bila kudhuru maslahi yako.
6) Jilazimishe kufuata ratiba yako.

NAMNA YA KUJIANDAA NA MTIHANI.
Maandalizi bora kabla ya mtihani ni kujisomea kwa njia zinazoleta matunda mazuri. Na zifuatazo ni baadhi ya njia zinazoweza kuleta mafanikio katika mitihani:
1. Jiandae mapema kwa ajili mtihani.
2. Jisomea kila siku kwa mujibu wa ratiba.
3. Ikiwezeakana jisomee na wenzako (weka kambi ya mtihani).
4. Pitia vizuri masomo yote.
5. Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kupunzika ili usipate kihoro au homa ya mtihani.
6. Kula vizuri, fanya mazoezi ya mwali ili uwe mchangamfu.
7. Usiku wa mtihani jisomee kwa muda wa masaa yasiozidi matatu, kisha pumzika vizuri na ulale kiasi cha kutosha.
8. Fika mapema katika chumba cha mtihani, robo saa kabla ya kuanza mtihani.
9. Soma vizuri karatasi ya mtihani kwa ukamilifu, na jaza sehemu husika kama inavyotakikana. Usisahau, kuandika namba ya mtihani, jina, tarehe na mambo yote muhimu.
10. Hakikisha unasoma maswali kikamilifu na kuyaelewa vizuri na kama hujayaelewa muulize msimamizi akupe ufafanuzi.
11. Anza kujibu maswali mepesi kabla ya magumu, kama taratibu za mtihani zinaruhusu kufanya hivyo.
12. Baada ya kumaliza kujibu maswali yote, tafadhali yapitie majibu yako yote kwa ukamilifu.
13. Usiwe na pupa ya kutoka nje ya chumba cha mtihani.
14. Soma kwa mara ya mwisho majibu yako,na utakapokuwa na uhakika ya ulichokiandika peleka karatasi yako kwa msimamizi wa mtihani na tia saini ya kuhudhuria.
NAMNA YA KUISHUGHULIKIA MISAMIATI MIGUMU:

Kwa hakika wanafunzi wa kigeni (yaani wale wanaojifunza kwa lugha zisizo za asili yao) wanakabiliana na changamoto za maneno magumu. Ili kujaribu kutatua tatizo hili, karatasi hizi zimejaribu kuanisha baadhi ya njia za kumsaidia mwanafunzi aweze kutatua tatizo la misamiati migumu kwa upande wake. Kwanza kabisa kabla ya kuelezea namna ya kupata maana za maneno magumu tunapenda tuzingatie yafuatayo.

MAMBO YA KUZINGATIA:
1. Usipendelee kutafuta maana ya maneno magumu katika kamusi kwani kamusi linaweza kukukatiza katika kusoma kwako. Tafadhali jaribu kutumia muktadha wa maneno (mtiririko wa tungo/sentesi) kujipatia maana ya maneno magumu kwani hilo litakusaidia kuendelea na kusoma bila kukatisha.
2. Unapopata maana ya neno kwa kupitia muktadha wa maneno, tafadhali liweke alama kisha, ukimaliza kusoma, litazame hilo neno katika kamusi na ulinganishe maana uliyoipata na ile ya katika kamusi. Kama itawezekana tumia kamusi maalum za istilahi za somo husika.
3. Kama hukufanikiwa kupata maana ya neno kupitia njia ya muktadha wa maneno, hapo ndipo unapotakiwa kutumia kamusi. Baada ya kuona mazingatio haya, sasa tutazame njia za kupata maana ya maneno magumu.

A: Njia za kupata maana ya maneno magumu:
I. Kwanza liwekee alama neno gumu kisha soma aya/ibara nzima hapo unaweza kupata maana yake. Na kama hujaipata, jaribu kuendelea na kusoma huenda maana yake ukuipata katika mistari ya mbele.
II. Kutumia kamusi. Ukiwa umeshindwa kabisa kupata maana ya neno kutokana na maelezo yaliyoandikwa katika kitabu husika, tumia kamusi kwa umakini, kwani mara nyingi kamusi inatoa fasili mbalimbali za neno husika.

B: Kupata maana ya neno kwa kupitia viashirio vya muktadha:
I. Wakati unasoma kitabu kwa lugha ya kigeni kisha ukakumbana na neno gumu, njia sahihi ya kutambua maana ya neno hilo ni kwa kupitia viashirio vya muktadha wa maneno.
II. Na muktadha wa maneno maana yake ni mazingira ya neno katika tungo au sentesi yenye kuonesha uhusiano wake na maneno mengine. Kwa Mfano neno meza kwa wale wasio waswahili, likitokea katika sentesi kama hii:
Tafadhali usikae juu ya meza. Hapa muktadha unaanisha kuwa neno meza hapa lina maana ya nomino (jina) la samani/fanicha iitwayo meza. Wala halina maana ya meza kitenzi (kitendo) cha kula na kumeza kitu kinacholiwa.
III. Viashirio vya muktadha wa maneno maana yake ni maneno mengine yaliyopamoja na hilo neno gumu katika tungo. Tukichukulia mfano uliopita utaona maneno usikae juu ya yanaashiria samani/fanicha. Wala hayaendani na neno meza kwa maana ya kumeza chakula.

AINA ZA MUKTADHA WA MANENO.
Fasili:
Wakati mwingine sentesi zinatoa fasili ya neno gumu. Mfano: ukikuta imeandikwa Kompyuta ni mashine ya umeme inayohifadhia na kuchanganua taarifa zilizoingizwa. Kwa hakika hii si fasili ya kamusi lakini inakupatia maana na matumizi ya hilo neno kwa hapo lilipo.
Mifano:
Wakati mwingine neno gumu linafafanuliwa kwa kupigiwa mfano ambao unaweza kukupatia maana ya neno husika. Mfano: Kipa wa Ruvu staa apunguze mbwewe, kama za kuchezacheza na mpira katikati ya mstari wa goli, na kujifanya hakuuona mpira, kudaka kwa mkono mmoja na kujifanya kateleza.

Ufafanuzi:
Kutoa maelezo ya neno husika. Mfano: Mwanafunzi mchecheto, yaani yule anayejikojelea kwa kuhofia mtihani anapaswa apewe ushauri nasaha.
Visawe: (mutaraadifaatu/sinonim)
Kisawe ni moja kati ya maneno mawili au zaidi yanayokaribiana sana kimaana. Mfano: Inasemekana huyo Mwizi hakutambua au hakujua kama nyumba ile inalindwa kwa kamera maalum.

Kwa ibara nyingine:
Ibara ni kifungu cha maneno au habari iliyokamilika, mfano: Tume ya haki za binadamu imefichua nyeti za mauaji ya kimbari, kwa kuziweka wazi siri za mauaji hayo.

Vinyume:
Kinyume ni neno lenye kukinzana na neno lingine. Mfano: mtu mwenye huzuni hana furaha hata kidogo.

Kutafakari:
Watu wengi wanapata kihoro wanapokutana na simba mbugani. Mtu anayetatafakari sana anaweza kujua maana ya kihoro kwa ktazama muktadha wa tungo hii.
Pia unapaswa kuzingatia muktadha wa neno wakati unapotazama fasili yake kutoka katika kamusi.
Na kama hujapata maana ya neno tafadhali litazame katika katika kamusi.
NAMNA YA KUJISOMEA VITABU VYA KIADA (SHULE):

Suala la kujifunza kwa kiasi kikubwa linafungamana na kusoma vitabu, kwa hiyo, tumeonelea tuzungumzie suala la kujisomea vitabu vya kiada kwa njia ya ufanisi zaidi.
Kwa bahati mbaya wanafunzi wengi wanajisomea vitabu vya kiada kama wanavyosoma vitabu vya riwaya au visa. Yaani wanaanza kusoma ukurasa wa kwanza na kuendelea kusoma moja kwa moja hadi ukurasa wa mwisho. Wakati kwa hakika hii si njia nzuri ya kusoma vitabu vya kiada. Kwani vitabu vya kiada vimeandikwa kwa lengo la kufundisha masomo yaliyomo ndani yake. Na vitabu vya kiada vimegawanywa kwa sura.
Na kila sura imegawanywa katika vitengo, na kila kitengo kina anuani yake. Na hii ni tofauti na vitabu vya riwaya ambavyo vimeandikwa kwa mtiririko mmoja kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kwa hiyo yapasa kuzingatia kuwa anuani za vitabu vya kiada ni nukta muhimu zinazoonesha kitabu kinafundisha nini na katika ukurasa gani. Kwa hiyo, ni jambo zuri kusoma vitabu vya kiada kwa njia maalum kama walivyoibainisha wataalamu.

Njia tuliyoichagua kwa ufipisho inaitwa (KUSUKH), na kirefu chake ni:
• K ----- Kagua:
• U ----- Uliza:
• S ----- Soma:
• U ----- Uliza:
• K ---- Kariri:
• H ---- Hakiki:

Jinsi ya kuitumia njia ya KUSUKH
1. Kagua: Kabla ya kuanza kusoma, tumia dakika mbili tatu kukagua kile utakachosoma. Hapa tunamaanisha kuwa, soma anuani zote za kifungu utakachokisoma.
Pia hakikisha unasoma muhtasari wa kifungu hicho kama upo. Vilevile soma maswali ya kujikumbusha yaliyoambatanishwa na kifungu hicho kama yapo. Faida ya kufanya hivyo ni kupata fikra ya kile utakachokisoma. Kumbuka faida za kukagua kitu kabla ya kukitumia.
2. Uliza: Baada ya kukagua, hatua inayofuata ni kuunda maswali ya kukusaidia kusoma kwa ufanisi. Na namna ya kuunda hayo maswali ni kama ifuatavyo: Geuza kila anuani iwe swali. Unaweza kuuliza kwa kutumia maneno yafuatayo: Vipi, lini, wapi, nani, inahusu nini, inafanya nini, muda gain nk. Kwa hakika ukibadilisha anuani na kuzifanya kuwa maswali, hilo linakusaidia kutambua wataka kufanya nini na kwa wakati gani.
3. Soma: Hatua ya tatu unatakiwa usome kwa makini kifungu chote ili upate majibu ya yale maswali uliojiuliza katika hatua ya pili.
4. Uliza: Baada ya kusoma, unda maswali mengine yanayohusiana na ufafanuzi uliotolewa katika kifungu. Kwa hakika maswali yanakupa changamoto za kufahamu na kukumbuka kile ulichokisoma.
5. Kariri: Katika hatua hii, unatakiwa uyarudie yale maswali uliyoyatengeneza pamoja na majibu yake uliyoyapata katika kusoma kifungu husika. Yaani soma maneno yale yale kimoyomoyo au kwa sauti au fanya vitendo vile vile mara kwa mara, rudia rudia.
Ni vizuri kuandika kwa ufupi maswali na majibu ya kifungu husika, kwani imethibitika kuwa kuandika kunasaidia kufanya mtu ashike vizuri zaidi kile alichokisoma au kukisikia. Pia waweza kutumia maandishi hayo kwa kujiandaa na mtihani yakiwa ndio ufupisho.
6. Hakiki: Hatua ya mwisho ni kufanya uhakiki wa kile ulichojifunza kwa njia ya kusoma. soma maandishi kwa kuyachambua na kufafanua mambo mbalimbali yaliyomo. Funika kitabu na karatasi ya majibu, kisha jiulize yale maswali ya kifungu cha pili, na jaribu kujipima je, unaweza kuyajibu? Kama jibu ni ndio hongera, hata hivyo soma tena katika kitabu ili kuhakikisha kweli umejibu sahihi. Kama jibu ni hapana bado una nafasi, rejea kusoma kurasa za majibu yako na kitabu ili kujiimarisha.

VIDOKEZO KATIKA KUTUMIA NJIA YA KUSUKH.
1. Tumia akili katika kuunda maswali, jiulize maswali ya msingi sio mzaha mzaha, uliza maswali, kabla na baada ya kusoma.
2. Uliza maswali ya kifungu chote.
3. Kabla hujaanza kuandika majibu ya maswali uliyojiuliza, hakikisha umeshasoma kifungu chote.
4. Andika kwa kutumia maneno yako, yaani kwa ufahamu wako. Pia fanya vifupisho kwa mtindo utakaouonelea kuwa unakufaa.
5. Usijihangaishe kwa kuandika majibu marefu, bora kuandika maneno mawili matatu yanayokukumbusha tu, kwani wewe hurudii kuandika kitabu!
6. Kumbuka kuwa hayo majibu na ufupisho ni wako, kwa hiyo usihofu kuwa watu wengine hawatoufahamu.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUJIFUNZA:

1. Jiwekee malengo ya kile unachotaka kukijua, pia jikadirie muda wa kutimiza malengo yako.
2. Wakati unapoanza kujifunza jiulize haraka haraka, Kitu gani unachokijua kuhusiana na kile unachojifunza? Kisha jiulize, wataka kujua kitu gani?
3. Ukimaliza kazi za kila somo, tafadhali rudia kile ulichojifunza kisha ieleze nafsi yako kile ulichojifunza ukiwa kama vile wamweleza mtu mwingine.
4. Jaribu kutambua baina ya masomo unayoyafahamu vizuri ukijifunza peke yako, na yale ambayo huyaelewi ukiwa peke yako.
5. Jaribu kujiwekea muda mzuri, wa kujifunza, muda ambao unakuwa makini sana, wala husinzii. Kisha utumie muda huo kwa kujifunza.
6. Jaribu kujifunza kwa muda wa dakika 30 hadi 60 kisha punzika kwa dakika 5 hadi 10 ndipo uanze tena kujifunza.
7. Ukifanikiwa kujifunza kitu na kukifahamu vizuri jipongeze pale unapopunzika kwa kufanya kitu kinachokufurahisha.

MAZINGIRA YA KUJIFUNZA.
Mazingira ya kujifunza ni kila kitu kinachomzunguka mtu anayejifunza. Ili kujifunza kwa ufanisi inatakiwa kuwepo kwa mazingira mazuri ya kujifunza, na ili kulijua hili tutazame nukta zifuatazo:
• Chagua sehemu ambayo unahisi kuwa wajisikia raha kama utajifunza ukiwa sehemu hiyo. Ni vizuri sehemu hiyo isiwe na watu wengi wanaokatisha ujifunzaji wako.
• Wakati unajifunza jaribu kuondosha vitu vyote vinavyoondoa mazingatio yako, kama vile, Tv, Redio, Kumpyuta, Dirisha lililowazi, makelele nk.
• Waeleze jamaa zako wasikusumbue wakati unapojifunza, kama hakuna jambo la msingi.
• Baadhi ya watu wanaweza kujifunza katika mazingira yasio tulivu, watu kama hawa wamebarikiwa, nao ni watu wenye sifa za kipekee kwa hiyo sio watu wa kuigwa.

KUSIKILIZA KWA UFANISI.
Kwanza kabisa tunapenda ifahamike kuwa kuna tofauti kati ya kusikia na kusikiliza. Kusika kunatokea bila kukusudia ama kusikiliza kunatokea kwa kukusudia. Kwa ibara nyingine, kusikiliza maana yake ni kuweka mazingatio katika kile unachokisikia na kujaribu kufahamu kile unachokisikiliza. Kwa faida yako, jua kuwa, kusikiliza kwa ufanisi ni elimu.
Na wataalamu wamesema kuwa: Msikilizaji mwenye ufanisi ni yule anaetoa mazingatio na mawazo yake yote kwa kile anachokisikiliza. Kwani msikilizaji mzuri ni yule anaesikiliza yanayosemwa na kuyatafakari.
Njia nzuri ya kukufanya utafakari kile unachokisikiliza ni kujiuliza maswali yanayohusiana na kile unachokisikia kisha kuyajibu kikamilifu.

Pia kuna baadhi ya wanafunzi hawapati faida inayotakiwa wakati wa kumsikiliza mwalimu na hii inatokana na sababu nyingi, miongoni mwazo ni:
1. Kutokuwa na hamu ya kusikiliza.
2. Kutojiandaa kwa ajili somo husika.
3. Kutotofautisha kati ya mambo ya msingi na yale yasiokuwa ya msingi wakati wa kusikiliza.
4. Kutokuwa na uhodari wa kusajili nukta muhimu wakati wa kusikiliza mada.

Ili kutatua matatizo haya inapasa kuzingatia yafuatayo:
1. Jiandae mapema kwa kile utakachokisikiliza.
2. Jaribu kukifanyia ufupisho na kujikumbusha kile kilichosemwa.
3. Jiulize zile nukta muhimu katika mazungmzo hayo.
4. Jaribu kumtafakari mzungmzaji ukiwa unamsikiliza.
5. Jaribu kukadiria mzungumzaji anaelekea kusema nini.
6. Jaribu kusikiliza kwa kufuatilia kile kinachoelezwa wazi wazi na mzungumzaji pia kile anachokificha.
7. Mtazame mzungumzaji wakati akizungumza, pia jaribu kuchunga harakati zake.
8. Sikiliza kile kinachosemwa kabla ya kukikosoa au kukiunga mkono. Yaani kwanza sikiliza hadi mwisho kisha unaweza kukosoa au kusifu. Kwani ukikatiza mazungumzo yake unaweza usisikie kile anachoendelea kukisema.
9. Jaribu kujizuia kongea na wasikilizaji wengine wakati mzungumzaji akiendelea kuwasilisha mada ili usiishughulishe akili na mambo yaliyo nje ya mada.
10. Andika nukta muhimu ukiwa wataka kukumbuka kile anachokisema mzungumzaji.
11. Sikiliza kwa kuzingatia ushahidi unaotolewa, na hili litakusaidia kuelewa somo husuka au hotuba nk.
12. Zingatia dhana ya msingi ya mzungumzaji wakati wa kumsikiliza.
MWONGOZO WA KUJISOMEA:

Kujifunza kwa ufanisi ni jambo muhimu sana. Sisi Tukiwa kama wanafunzi, tunasumbuliwa na matatizo mengi ya kiuanafunzi, ambayo sote tunayajua. Hata hivyo, pongezi kwa Uongozi wa TSU EGYPT kwa kuamua mwaka huu uwe mwaka wa kuandaa na kuwasilisha tafiti za kielimu zinazohusiana na maswala mbalimbali yanayowagusa watanzania. Nyaraka hizi zina shabaha ya kuchangia katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo la Kujifunza kwa ufanisi.

Kwa hakika, wengi wetu, tunachukulia kuwa, Kujifunza ni kwenda vyuoni au madarasani. Hayo ni mojawapo ya mawazo finyu kuhusiana na kujifunza, kwani kujifunza kuna maana pana zaidi kuliko ile ya kwenda madarasani.
Ili tusirefushe sana! Kujifunza kunakusanya kwenda madarasani na kuwasikiliza wahadhiri kwa makini, kujisomea vitabu na makala mbalimbali kwa ufanisi, kusikiliza marafiki, walimu, wazazi, wataalamu, kutazama video, sinema, kufanya utafiti (bahthi/research), kufanya kazi za nyumbani, kufanya mazoezi, kufikiria njia za kutatua matatizo, kufikiria njia za kujiletea maendeleo, nk.
Kwa faida ya msomaji/msikiliza: Jaribu kuweka akilini huu ufahamu mpana wa kujifunza kwani hilo litakusaidia kujifunza kwa ufanisi na kwa maendeleo endelevu.

Baada ya utangulizi huu linaibuka swali! Mbinu za kujisomea ni nini? Mbinu za kujisomea ni mfumo au njia za kumfanya mtu ajifunze kiwepesi na kwa ufanisi zaidi. Tunapenda ifahamike kuwa hizi Mbinu za kujifunza sio kitu mbadala cha kuacha kutoa bidii katika kujifunza.
Kwa hakika juhudi katika kujifunza ni jambo la muhimu sana. Ama umuhimu wa mbinu za kujifunza ni kuwepesha na kurahisisha suala la kujifunza. Pia zinaokoa muda na nguvu za mwenye kuzitumia. Imesemekana kuwa: Watu wanajifunza na kufahamu vizuri pale wanapotekeleza kivitendo yale wanayojifunza.
Kwa mfano ukimfundisha mtu kuendesha baiskeli atajua haraka kama atakuwa amepanda baiskeli sio maneno matupu! Au kama vile kumfundisha mtu kuogelea akiwa nchi kavu kwa kweli hatoweza kujua kuogolea. Pia ieleweke kuwa kila mtu anajifunza kwa njia yake anayoipenda na kuona inamfaa.

Monday 30 January 2012

SOMO LA FIQH (DARASA LA KWANZA):

Najsi na namna ya kujitwaha-risha.
• Vitu vilivyonajisi.
• Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
• Adabu za kwenda haja.
• Kujitwaharisha baada ya kwenda haja

MBINU ZA KUFUNDISHIA.
• Kwa njia ya maelekezo na kumuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi umuhimu na faida ya usafi.
• Mwalimu awaelekeze wanafunzi kwa vitendo namna ya kupiga mswaki, kukoga, kuchana nywele, kufua, kupiga pasi, n. k.
• Mwalimu kila mara awakague wanafunzi kwa usafi na unadhifu wa mwili na nguo.
• Awafahamishe wanafunzi faida za usafi na hasara za uchafu.

VIFAA VYA KUFUNDISHIA.
• Nguo chafu na safi.
• Miswaki
• Sabuni
• Kitana
• Kikata kucha n. k.

LENGO.
Ajue kuwa usafi ni sehemu ya Uislamu.

Kutawadha:
MBINU ZA KUFUNDISHIA
• Mwalimu awaelekeze wanafunzi kutawadha kwa vitendo na awape wanafunzi mazoezi ya kutawadha mmoja mmoja mbele ya darasa.
• Aorodheshe ubaoni yale yanayotengua udhu na kuwataka wanafunzi wayarudie.

VIFAA VY KUTUMI.
• Ndoo ya maji
• Makopo
• Kata, n. k.

LENGO.
• Aweze kutawadha
• Aweze kutaja yanayotengua udhu

AKHLAQ:
MBINU ZA KUFUNDISHIA.
• Kwa njia ya maelekezo na kumuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi umuhimu na faida ya usafi.
• Mwalimu awaelekeze wanafunzi kwa vitendo namna ya kupiga mswaki, kukoga, kuchana nywele, kufua, kupiga pasi, n. k.
• Mwalimu kila mara awakague wanafunzi kwa usafi na unadhifu wa mwili na nguo.
• Awafahamishe wanafunzi faida za usafi na hasara za uchafu.

VIFAA VYA KUTUMIA.
• Nguo chafu na safi.
• Miswaki
• Sabuni
• Kitana
• Kikata kucha n. k.

LENGO
Ajue kuwa usafi ni sehemu ya Uislamu

ADABU ZA KULA:
MBINU ZA KUFUNDISHIA.
• Mwalimu awafahamishe wanafunzi vyakula vya halali akizingatia umri wao.
• Kwa njia ya maelekezo na kuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi vyakula vizuri vinavyokamilisha mlo na umuhimu wake katika mwili kulingana na umri wao.
• Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa vitendo namna ya kula kwa taratibu za Kiislamu.

VIFAA VYA KUTUMIA.
• Chakula
• Ndoo ya maji
• Ndoo tupu
• Glasi za maji, n.k.

LENGO.
Aweze kula kwa kuzingatia Sunnah
SOMO LA FIQH (DARASA LA KWANZA):

NGUZO ZA UISLAMU.
• Kutoa Shahada
• Kusimamisha Swala
• Kutoa zaka
• Kufunga Ramadhani
• Kuhiji Makka kwa mwenye uwezo.

MBINU ZA KUFUNDISHIA.
• Mwalimu ataje nguzo tano – moja moja kisha wanafunzi wamfuatishie kwa kundi kisha mmoja mmoja. Atumie Hadithi “Buniyal Islamu alaa khamsin….”.
• Mwalimu awawezeshe wanafunzi kutamka, kuandika na kutafsiri shahada mbili kwa kuwazoesha kutamka na kuandika shahada na tafsiri yake • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kuwa maana ya shahada ni kufuata maamrisho na makatazo yote ya Allah (S.W.) na Mtume wake. • Mwalimu abainishe maamrisho na makatazo ya Allah na Mtume wake kulingana na umri wa wanafunzi. • Wanafunzi wenyewe wataje nguzo tano katika kundi, kisha mmoja mmoja.

KUTOA SHAHADA.
• Kutamka na kuandika Shahada
• Kutafsiri Shahada

VIFAA VYA KUFUNDISHIA.
• Picha ya nyumba Yenye nguzo tano

LENGO.
Aweze kutaja nguzo za Uislamu.
Aweze kutamka na kuandika shahada
Aweze kutafsiri shahada
SOMO LA TAWHIDI(DARASA LA KWANZA:

Kuwepo kwa Allah (S.W.). Mwalimu awaulize wanafunzi maswali yatakayowapelekea kuyakinisha kuwepo kwa Allah (S. W.) kwa kutumia mazingira yao
VIFAA VYA KUTUMIA.
• Jua.
• Mwezi.
• Nyota.
• Mawingu.
• Kitabu cha I (IPC).

LENGO.
Mwanafunzi aweze kupambanua kuwepo kwa Allah (S. W.) kutokana na mazingira yake (Allah ni muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo).

KUSOMA QUR-ANI (DARASA LA KWANZA:

Kusoma kwa ufasaha sura ya:-
• Al-Fatiha mpaka Al- A’laa
• Kuhifadhi sura hizo
• Kuandika
o Al-Fatiha
o Annas
o Al-Falaq
o Al-Ikhlas

• Mwalimu awasomee wanafunzi sura huku wakisikiliza kisha awaamuru kusoma katika kundi kisha mmoja mmoja.
• Mwalimu awawezeshe wanafunzi kuhifadhi kwa kumfuatisha bila kuangalia kitabuni kwa kundi na kisha mmoja mmoja.
• Mwalimu aandike ubaoni sura anayosomesha.
Mwalimu awaamuru wanafunzi kuandika al-Fatiha, annas, Al-Falaq na Ikhlas.

VIFAA VYA KUTUMIA.
• Ubao na chaki.
• Vibao vya wanafunzi.
• Radio kaseti.
• Kitabu cha I (IPC).

LENGO (MWANAFUNZI).
• Aweze kusoma Qur’an kwa ufasaha na kuhifadhi.
• Aweze kuandika Al-Fatiha, Annas, Alfalaq na al-Ikhlas.
MBINU ZA KUFUNDISHIA (DARASA LA KWANZA).
KUTAMBUA, KUANDIKA NA KUSOMA HERUFI ZA QUR-ANI:

• Mwalimu awaonyeshe na kuwatamkia wanafunzi herufi mojamoja Atumie picha na kadi.
• Wanafunzi wamfuatishe Mwalimu kutamka herufi moja moja kwa wote kisha mmoja mmoja.
• Wanafunzi wafanye mazoezi ya kuandika herufi moja moja katika ardhi, ubaoni, katika karatasi ngumu, n.k.
• Mwalimu awatambulishe wanafunzi hatua kwa hatua alama za Irabu, tanwin na sakna na atoe mazoezi ya kutosha ya kusoma na kuandika herufi za Kiarabu zikiwa na alama hizo.
• Mwalimu awaonyeshe herufi moja moja inavyokuwa ikiwa inaungwa mwanzoni, katikati na mwishoni mwa neno. Abainishe herufi zisizoungika na atoe mazoezi ya kutosha ya kusoma na kuandika.
• Mwalimu awatambulishe wanafunzi alama za madda na shadda na zinavyotumika katika kusoma•
• Mwalimu atoe mazoezi mengi ya kusoma na kuandika.

LENGO (MWANAFUNZI)Aweze kusoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu.

VIFAA/REJEA.
• Ubao na chaki.
• Kadi za herufi.
• Kadi za maneno.
• Mbao/ubao.
• Juzuu Amma.
• Kitabu cha I (IPC).
NINI CHA KUFANYA ILI TUSOMESHE NA TUSOME HIZI ELIMU ZA KI-SECULAR, KWA MPANGO WA KIISLAMU??

1. Walimu Waislamu wa mashuleni wajitolee kuandika masomo ya shuleni bila kubadilisha syllabus kwa mpango wa kiislamu.
Kila Sura (chapter) iwe na utangulizi wa aya za Qur-ani na Hadithi kuhusu Sura hiyo, na ndani ya Sura hiyo pia, kuweko na aya ya Qur-ani na Hadithi.
Sura hizo pia zitoe mchango wa Waislamu kwenye somo hilo, bali kwenye kipengele hicho pia.

2. Kuwe na masomo ya dini kwa uhakika wa masomo hayo. Masomo hayo ni kama sheria ya Kiislamu, Sira, Tabia na mambo ambayo yanamuathiri Muislamu kila siku.
Isiwe kama shule zetu, tunamfundisha mtoto wetu jinsi ya kutoa hoja za dini, jinsi ya kujibizana na kafiri na asiye na dini lakini ukimwuliza jinsi ya kuswali, hajui, akienda chooni anajisafisha vipi, hajui. Wakati haya ndio masuala muhimu zaidi kuliko kujua kutoa hoja.

3. Walimu waambizane wenyewe kwa wenyewe umuhimu wa suala hili, walitangaze na kuliendeleza suala hili, na kila mmoja afanye kilicho kwenye uwezo wake.
Kila mtu afikishe ujumbe kwa mwenziwe, mwenye elimu atoe mchango wa elimu, mwenye pesa atoe mchango wa kuchapisha vitabu, mashule na kadhalika.

4. Ikiwa tutasubiri mpaka tuunde Chama, Kamati, Jumuiya ambayo itashughulikia suala hili, hatutafika popote. Tunajua udhaifu wetu, kila mmoja atakuja na makusudio yake, wengine watakuja ili wajaze mifuko yao na matumbo yao, wengine watakuja ili wapate umaarufu, na wengine watawekwa na vikundi ambavyo si vya Waislamu ili waharibu hiyo Jumuiya na mwisho tutavunja Jumuiya yetu.
Mwenyezi Mungu atupe uwezo wote, wa kuutumikia Uislamu na Waislamu kwa njia bora na ambayo anairidhia Yeye - Aamin.”
MAFUNDISHO YA SHULE KWA MPANGILIO WA KIISLAMU:

“Uislamu ni tajiri sana kwenye upande wa elimu na hakuna elimu ambayo imeiacha. Hivi karibuni tutatoa mwelekeo wa uislamu kwenye elimu, na tutanukuu maneno ya Imaam Ghazali kwenye Ihyaa Uloomud-Diin. Tutatunukuu hapa sehemu ndogo kwa kifupi sana, Imaam Ghazali anasema elimu imegawika kuwa lazima kwa kila mmoja, na elimu iliyokuwa lazima kwa kikundi cha watu, elimu iliyokuwa makruuh na elimu iliyokuwa mubaah na elimu iliyokuwa haramu.

Katika elimu iliyokuwa lazima, kasema si lazima mtu ajue milango yote ya sheria bali ajue kila kinachotakiwa katika muda na hali alionao, akasema kwa mfano si lazima kujua hukumu za Hijja kama hana uwezo na wakati wa Hijja haujafika.
Kisha akaendelea kueleza na akasema watu wanahangaika kusoma maelezo ya undani wa sheria na mifano ya mas-ala ambayo hayatokei ila kwa nadra na wakati mjini kwao hakuna daktari wa kike Muislamu wa kutibu wanawake wa kiislamu, na ni jambo la lazima kwa wakazi wa mji na kama halijafanyika wanapata madhambi wakazi wote.

Kwa hiyo ni wazi kuwa baadhi ya elimu tunazoziita za dunia ni lazima tujifunze kwa amri ya dini yetu, na tusipofanya hivyo tutaingia kwenye madhambi makubwa. Maelezo zaidi tutayatoa kwenye makala zetu zijazo.
Wajerumani walivyokuja Tanganyika, wakaona wasomi zaidi ni Waislamu, wanajua kusoma na kuandika, wanajua hesabu na wanatumia tarakimu za kiarabu kwenye maandiko yao, hata lugha ya Kiswahili ilikuwa wanatumia maandishi ya kiarabu. Wakawaajiri hawa kwenye mahakama, na nafasi za Serikali.

Mwingereza alikuja na makusudio yake, ya kuuvunja uislamu na kuwadhoofisha Waislamu, akajenga mashule na kuweka masharti anayetaka kujiunga lazima awe mkristo, ili ajiunge, ndiyo wakati tuliopata majina ya Augostino Saidi na mengineyo.
Waliopenda dini yao, wakachukia masomo ya kizungu na kukataa kupeleka watoto wao mashuleni, ili wasiwe wakristo, wakahifadhi dini yao, lakini ikajijenga tabia ya kuchukia elimu za kizungu.

Kwa hakika elimu hizi si za kizungu, ni za Waislamu wenyewe na zinarudi kwao wenyewe, Waislamu waliendeleza elimu na teknolojia, na wafalme wa kiislamu waliwapa zawadi kubwa kubwa wasomi waliovumbua mashine mpya, na zawadi ya kanisa ilikuwa ni kuwaua wanasayansi.
Hapo ndipo wakazi wa nchi za kizungu wakaamua kuweka mbali dini na sayansi & Teknolojia. Kitu hicho hakipo kwenye Uislamu. Ndiyo elimu ya secular ilipoanza.

Tukirudi kwenye Tanganyika, nafasi za Serikali zikaanza kuchukuliwa na wakristo, na wakaendelea kupata nafasi hizo, hadi Waislamu walivyoanzisha TANU, hawakuwa na Muislamu wa kushika nafasi ya juu kabisa na kumweka mkristo kwenye nafasi hiyo, na hatimaye wakristo wakaendelea kutawala.

Hiyo ni historia, tusiisahau, lakini pia isiwe ni sababu ya kutupia lawama zote kwa historia, sisi tumefanya nini kuibadili historia hiyo? Waislamu bado kwa asilimia kubwa sana wanachukia elimu za kizungu, na wana hiari wawasomeshe madrasa tu, wasipate elimu za kizungu, au wawasomeshe elimu za kizungu na wasipate elimu za dini, kama wanavyotoka Waislamu wengi hata kwenye shule tunazoziita za Kiislamu.
Hakuna sehemu ambapo tumeziweka hizi elimu za kizungu ambazo kwa hakika si za kizungu ziendane na mafunzo ya Uislamu, na kama zipo shule hizo labda hatuzijui.

Kwa kweli njia hizi mbili tumeziweka mbali sana, na hatujajenga njia ya kuzikutanisha, Wanasayansi wakubwa wa kiislamu, wanaanza vitabu vyao kwa Bismillahi, kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume - Rehema na Amani zimshukie - na bado wanabaki kuwa wanasayansi na wavumbuzi na wazungu wanaiba uvumbuzi wao na kusema wamevumbua wao, bali kushika kwao dini kunawafanya wawe wanasayansi wakubwa zaidi.

(f) NJIA ZA KUFUNDISHIA QUR-AN KWENYE MADRASA ZETU:

Njia na mbinu pamoja na mikakati mbali mbali ni muhimu sana katika ufundishaji wa usomaji Quran katika madras zetu, vinginevyo mtoto atasoma muda mrefu sana ili kuelewa. Baadhi ya mbinu za kufundishia ni pamoja na kusoma herufi bila irabu kwa njia ya ubao, kadi, daftari n.k.

MUHIMU:
- Mwalimu afundishe kwanza herufi bila irabu. Yaani: ALIF, BE …….
- Kisha afundishe Irabu. Yaani: FAT’HA, KISRA, ……
- Afundishe kuchanganya herufi hizo pamoja na irabu zake; Mfano: BE FAT’HABA, TE FAT’HATA …….
- Mwalimu atumie michezo kadhaa kwa watoto kuzitambua herufi.

Mfano: NGAZINGAZI, KIKAPU, UPANGAJI, GURUDUMU ZA GARI, NYUMBA …. n.k.
- Mwalimu afundishe kuchanganya SILABI ili kupata neno. Ni vizuri Mwalimu akaanza na kinachoeleweka kwenda kisichoeleweka.

Mfano: Kumwezesha motto kuandika BABA kwa herufi za Kiarabu, kasha aandike neno la kiarabu kwa herfu hizo.

HITIMISHO
Mwalimu anapaswa kujua anachokifundisha, pia kufahamu na kuweza kutumia njia na mbinu muafaka. Kwa kawaida hatupaswi kulenga kusema sana, au kueleza mengi, bali tulenge kuwezesha mengi kufahamika kwa urahisi zaidi.
Kwa muda mrefu MADRASA zimesahaulika na kusababisha athari mbaya.
Ili kuziendeleza tunapaswa kuzingatia kazi zinazotakiwa kufanywa na madrasa na zipi zinafanywa. Kuelewa tatizo kwa undani. Historia ya Madrasa Tanzania ni muhimu kufahamika ili kurudisha mzizi wa tatizo. Kadhalika, Matatizo yanayoikabili taasisi ya Madrasa na ufumbuzi wake ni muhimu vikajadiliwa.
Aidha , kuna haja ya kukumbuka taluma muhimu kwa walimu wa Madrasa na kuona kama wengi wanazo.
Kama si hivyo, basi mikakati iwepo kuwawezesha walimu wa Madrasa kuendesha madrasa zetu (Uendeshaji Madrasa) pamoja na kuwa na mbinu bora za kufundishia katika madrasah zetu.

Sunday 29 January 2012

SOLUHISHO KWA MADRASA ZETU:

- Ni vigumu kuliondoa tatizo hili kwa kulifanya jukumu hilo kuwa la watu Fulani tu.
Mfano, kulifanya liwe jukumu la masheikh tu, au jukumu la walimu tu, au la wazazi tu. Inapaswa kuwa ni tatizo linalomgusa kihisia kila muislam.

- Kwa hakika elimu hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya uislam na waislam kiimani(kiitikadi), kitaaluma, kielimu n.k.

Mfumo.
- Kuna haja ya kuudurusi mfumo wa elimu ya madrasa na kuangalia namna ya kuuendeleza na kuuboreha kwa manufaa ya kizazi cha kiislam.

- Mfumo wa madrasa zetu uendane kabisa na haja iliyopo katika jamii kwa lengo la kuwaendeleza watoto kitaaluma.

Walimu.
- Kuwepo na mpango maalumu wa kuwaendeleza walimu kielimu, kitaaluma na kiuchumi ili kuwaongezea hari ya kujituma na kutoa jitihada zote kwa ajili ya maendeleo ya taasisi hii muhimu, “madrasati”.
Mfano:
Kuwepo kwa makongamano na semina ili kuwawezesha walimu kushirikiana katika ujuzi na mbinu za kufundishia na kuendeshea madrasa zetu.

- Walimu wawe wabunifu kiuchumi ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendeleza madrasa zetu.

- Walimu wasijione kuwa wao ni waislam au watu wa daraja la chini sana kimaisha. Bali wajione wao ni watu muhimu kabisa katika jamii na kazi yao ni jukumu lao si jukumu la mtu Fulani na wala hawafanyi kazi hiyo ili tu kuwaridhisha watu Fulani bali ili kumridhisha allah (s.w).

Jamii ya Kiislam.
- Ifanye fikra juu ya jinsi ya kuboresha na kuendeleza madrasa zetu na watoto wetu katika taaluma muhimu za kiislam.

- Jamii nzima ieleweshwe juu ya nafasi sahihi ya Madrasa na Elimu ya Madrasa kwa maisha ya Waislam nchini.

Taasisi za Kiislam.
Zishirikiane kuona jinsi ya kutatua matatizo hayo.

TAALUMA MUHIMU KWA WALIMU WA MADRASA:

Kila nyanja inahitaji taaluma Fulani ili kuifanya nyanja hiyo iwe imara, bora, makini na yenye manufaa kwa maisha na ummah kwa ujumla. Hata Mitume (rehma na amani za Allah ziwafikie) walipewa taaluma maalumu kwa kazi zao. Katika maisha yetu tunahitaji taaluma zinazowezesha watu kutekeleza majukumu yao katika jamii na mazingira wanayoishi.

Mfano:
Mwalimu wa madrasa anahitaji taaluma juu ya;
(i) Uendeshaji wa madrasa.
(ii) Ufundishaji.
(iii) Saikolojia ya watoto na malezi.
(iv) Taaluma inazofundisha kama vile Fiqih, Tareikh, Qurani, Kiarabu, Tawhiid, Sirah, Akhlaq n.k.

Njia za kufundishia (Muhtasari)
Zipo njia kadhaa Bwana Mtume (s.a.w) amekuwa akizitumia katika kufundishia watu. Pia Quran imeeleza njia kadhaa kwa ajili ya ufundishaji. Kwa muhtasari njia hizo ni pamoja na hizi zifuatazo.

(a) Simulizi (Narration)
- Hii ni njia ambayo mwalimu anafundisha kwa kutumia visa vya kubuni au visa halisi. Njia hii inafaa sana kutumika hususan kwa watoto wadogo.

- Katika Quran njia hii imetumika kutufundisha mara kadhaa.
Kanuni na njia zenyewe katika Quran zimeelezwa katika “NJIA ZA KUFUNDISHIA KATIKA MADRASA ZETU”. Hapa ni muhtasari tu.

- Njia hii yaweza kutumika katika kufundisha Sira ya Mtume, Akhlaq, Tareikh, Fiqih hata tawhiid. Alimradi mwalimu afahamu jinsi ya kuitumia njia hiyo kwa ufanisi.

(b) Uelezeaji (Description)
- Njia hii hutumika kuelezea dhana au wazo Fulani katika uislam. Muhimu kwa mwalimu ni kuifahamu misingi ya njia hii pamoja na kuelewa mazingira yanayofaa kwa njia hii.
Mfano:
(i) Ili kutoa maf’hum(ufahamu) mzuri kuhusu “UISLAM” kama dini njia hii yafaa kutumika.

(ii) Ili kufundisha vizuri, mazingira ya vita vya Badr, Uhud, Khandaq n.k. kwa lengo la kufundisha mazingatio yanayopatikana, mwalimu aweza kutumia njia ya UELEZEAJI (Description)
- Kadhalika, cha muhimu ni maarifa kuhusu njia hii.

(c) Njia ya Uoneshaji (Demonstration)
- Ni njia inayotumika kufundishia mada zinazolenga kutoa ujuzi kwa wanafunzi kutenda matendo maalum:
Mfano:
(i) Swala ya mait.
(ii) Swala ya Faradh na Sunnah.
(iii) Kushona Sanda.
(iv) Kuosha Maiti.
(v) Kuchukua Udhu n.k.
- Mada kama hizi zikifundishwa pasipokutumia njia hizi, ueleo wa wanafunzi unaathirika.

- Mwalimu anatakiwa kuifahamu njia hii kwa madhumuni ya kuitumia kwa ufanisi.

(d) Njia ya ugunduzi na udadisi.
- Njia hii inamtaka mwalimu aoneshe tatizo kisha awaongoze wanafunzi katika kugundua suluhisho. Kwa kufanya hivi, milki ya ung’amuzi (Cognitive Facult) itakuwa imeendelezwa. Quran inasisitiza matumizi ya milki ya ung’amuzi (Cognition domain).
Mfano:
(i) Baada ya kufundisha “Tawhid” – Mwalimu anaweza kutoa habari ya kweli kuhusiana na tawhiid kisha wanafunzi wakajadili kwa mnasaba wa tawhid.

(ii) Mwalimu aweza kufundisha “Tareikh” – Hijar kutoka Makka kwenda Madina, alafu wanafunzi watatakiwa kugundua wanachojifunza.

(iii) Mwalimu anaweza kutoa tatizo liliopo katika jamii kwa mnasaba wa uislam, kisha akawataka wanafunzi waoneshe sababu na suluhisho.

(e) Njia ya Kuhifadhi.
- Hii ni muhimu sana katika elimu na maarifa ya kiislam. Mwalimu anatakiwa kuwawezesha wanafunzi kuhifadhi katika mada kadhaa.
Mfano:
(i) Katika Swala, mwalimu atumie njia rahisi kwa wanafunzi kuhifadhi.

(ii) Katika udhu, mwalimu atumie njia hii pia ili wanafunzi waweze kuhifadhi maneno muhimu.

(iii) Katika Dua, wanafunzi wahifadhishwe dua.

(iv) Katika Tarekh, wanafunzi wahifadhishwe aya na hadithi mbalimbali zinazonasibiana na matukio katika mada.
Mathalani, kufundisha Mkataba wa hudaybiya, Quran 48:1. 48:18 ni vema zikahifadhiwa.
Pia katika kufundisha AKHLAQ (Tabia) mwalimu awahifadhishe watoto, Sura ya 64.4 ikiwezekana, kulingana na umri wa watoto, Pia wahifadhi Quran 33:21.

Tuesday 24 January 2012

Kustawi kwa Elimu ya Madrasa Afrika Mashariki:

 Mwaka 1332, Mwarabu aitwaye IBN BATUTA alipotembelea Kilwa alikuta mji umekaliwa na waliokuwa wakitumia lugha ya Kiswahili.
 Baadaye miji ya Tanga, Dar-es-Salaam, Mombasa, Lamu, Malindi, na Mikindani vikawa vituo vya kueneza uislam na elimu ya kiislam katika miji ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Zaire, Msumbiji, Malawi na Burundi.

Maarifa yaliyotolewa na njia za kufundishia.

 Maarifa yaliyotolewa na kuonekana hayo ndiyo maarifa ya uislam ni pamoja na:
(i) Zipi ni nguzo za imani na maana yake.
(ii) Zipi nguzo za Swala na maana yake.
(iii) Namna ya kusoma Quran, lugha ya kiarabu na vira kadhaa.
(iv) Sirah ya Mtume (s.a.w)
(v) Kanuni zinazotawala utendaji wa Ibada Maalumu.

 Maarifa haya yalifundishwa kwa njia kuu ya Kipurure,(yaani Mwanafunzi hakusoma kwa njia ya kuuliza na kudadisi.

 Walimu wa kufundisha hayo, ni wale tu, walioonekana wanaweza kuyasoma hayo. Hakukuwa na mazingatio kuhusu uwezo na ujuzi wa mfundishaji kufikisha maarifa anayoyatoa.

 Kwa sababu hizo, pia njia kuu ya kudhibiti nidhamu, ilibaki kuwa ni viboko tu.
 Kwa ujumla taaluma kuu za elimu ya Madrasa zilizotawala ni KUSOMA, KUANDIKA, KUIFADHI na KUIGA ambazo zilitolewa na walioweza kuzipata taaluma hizo.

Dosari za Elimu ya Madrasa iliyotolewa wakati wa Waarabu.

 Dosari hizo zimetokana na asili ya kuenea kwa dini na elimu ya Kiislam Afrika Mashariki, hususan Tanzania.

 Tatizo linakuja kwa vile Uislam na elimu ya Kiisam:-
(i) Vilenea katika taratibu za walioeneza kujitafutia maisha yao wala si kwa madhumini ya kufanya umisionari.
(ii) Vilienezwa na waislam ambapo hawakuwa na maandilizi ya kufanya hivyo, hivyo hakukuwa na matayarisho yoyote ya malengo ya kielimu.
 Matokeo yake uislam ulifundishwa ili kupata wenzi na washirika katika masuala ya kijamii kama vile:
o Misiba
o Harusi n.k..

(i) Zilifundishwa Taaluma chache tu.
Mfano: Kusoma, Kuandika, Kukariri Quran.

Taaluma hizo si pana kiasi cha kuwawezesha wanafunzi kuuhami uislam kifikra au vyovyote, taaluma hizo hazimwezeshi mwanafunzi kumudu changamoto zinazoibuka kila kukicha; Japo uislam haushindwi na changamoto yoyote ile.

(ii) Njia za kuendeleza nidhamu, na maadili zilikuwa ni viboko tu, ukali tu, pasi na kuchunguza tatizo kwa lengo la kuondoa tatizo hilo na kusaidia.

(iii) Njia za kufundishia hazikuzingatia umuhimu wa kuendeleza na kuhusisha nyanja tatu za kujifunza.
(a) Nyanja ya ung’amuzi (Cognitive domain).
(b) Nyanja ya matendo (Psychomotor domain)
(c) Nyanja ya kuhusisha (Affective domain)

Kila nyanza hapo inaumuhimu katika uislam wa mtu mmoja mmoja au jamii na hatimaye Ummah.

(iv) Hakukuwapo chombo maalum cha kijamii, kinachosimamia swala zima la utoaji wa Elimu hii. Matokeo yake kila mmoja alifundisha kadiri na namna alivyodhani ni sawa.

Athari za dosari hizo
(i) Kukosekana kwa taaluma muhimu za kifiqih

Mfano:
- Taaluma inayowezesha kuhusianisha mazingira na fatwa kadhaa za kifiqih.
- Taaluma inayofafanua hukumu kadhaa za kifiqih na yanayotokea katika maisha.
Katika hili, kumekosekana taaluma ya kubainisha tofauti ya RIRA na HIBA.

(ii) Watu wachache sana ndio waliweza kuendelea na elimu ya Madrasa kwa kiwango cha juu kwa kulinganisha na waislam wengine.

Mfano:-
Ni Masheikh wachache waliweza kufikia kiwango fulani. Matokeo yake hata vitu vidogo vidogo kuweza kufahamika kwa waislam wote, vinafahamika na masheikh tu.

(iii) Kuibuka kwa Matabaka miongoni mwa waislam kutokana na dosari hizo,
kumeibuka matabaka kadhaa mingoni mwa waislam.

Mfano:
o Tabaka la wasomi wa elimu katika mfumo huu wa madrasa tu.
o Tabaka la waliosoma elimu ya madrasa kidogo na elimu ya kisekula kidogo.
o Tabaka la waliosoma kiasi elimu ya kisekula na kukosa elimu ya madrasa lakini badaye (ukubwani) wakajifunza elimu ya uislam kwa mfumo mwingine.

Mahusiano ya matabaka haya hayasaidii kuendeleza uislam na waislam kwa ujumla, ni sumu kwa maendeleo ya jamii ya kiislam.

MATATIZO YANAYOIKABILI ELIMU YA MADRASA TANZANIA:

Taasisi ya Madrasah inazidi kupoteza hata hadhi yake ndogo iliyokuwa nayo.

Mfano:
Jamii haiipi hata thamani inayostahiki licha ya kuwa madrasa ni taasisi muhimu katika kurithisha mila, destuli na mfumo mzima wa uislam toka kizazi hadi kingine. Wazazi na watoto wa kiislam leo hii hawana hari ya kupeleka watoto wao kwenye vituo vya madrasa. Wala wazazi hao hawana hata haja ya kujua mikati ya madrasa zinazowazunguka.

(ii) Matatizo.
Matatizo yanayoikabili elimu ya madrasa ni:
Matatizo ya Kitaasisi (Institutional Problems.
) (a) Hakuna mfumo wa uendeshaji elimu ya madrasa. Mfumo huo hautoi picha halisi juu ya nani hasa ndiye mratibu au msimamizi wa elimu ya Madrasa. Kwa sababu hiyo hakuna upimaji wala tathimini yoyote ili kuelewa kuwa nani anastahiki kuwa msimizi wa elimu hii muhimu.

(b) Kukosekana kwa “usare” (uniformity) katika ufundisjaji.
Matokeo yake anapohama mtoto kwenda madrasa nyingine anaathirika kitaaluma.

(c) Hakuna utaratibu fasaha/muafaka wa kuwahusisha wazazi wa Kiislam katika kujadili maendeleo na kutathimini uendeshaji wa madrasa. Athari yake ni wazazi kutojihusisha na uendelezaji wa madrasa zetu na ufuatiliaji wa taaluma muhimu zipatikanazo.

(d) Kukosekana kwa utaratibu wa kubadilishana mawazo baina ya waalimu tofauti tofauti, juu ya uboreshaji wa njia za ufundishaji na mafanikio katika uendeshaji madrasa.

(e) Kukosekana kwa mipango inayohusiana na madrasa, wanafunzi na walimu. Athari yake ni kupungua kwa idadi ya wanafunzi na walimu wa madrasa.

(f) Kukosekana kwa utaratibu maalumu juu ya vigezo vinavyomuwezesha mtu kuwa mwalimu.
Kwa kawaida yeyote anayejua kusoma na kuandika herufi za kiarabu, kusoma Quran na mambo kadhaa katika Ibada maalumu za kifiqih, aweza kuwa mwalimu hata kama sifa za kitabia, na uwezo wa kurithisha elimu kwake ni vikwazo.

TANBIH:
Aina za walimu zaweza kuwa kama ifuatavyo:-
(i) Mwenye sifa (Qualified) – Anazo sifa kitabia, anaweza kuwa na ujuzi wa kufundisha na ana elimu.
(ii) Mwenye sifa (Underqualified) – Anayo elimu ila hana mbinu bora za ufundishaji.
(iii) Asiye na sifa (Unqualified) – Hana sifa hata kidogo. Huyu ni hatari sana.

Matatizo ya Kijamii.
(a) Fikra za watu juu ya elimu ya madrasa na thamani yake
- Jamii na mtu mmoja mmoja wanachukulia elimu ya msingi ya madrasa ni kusoma Quran na kujua kanuni muhimu za utekelezaji wa Ibada maalumu kama vile Swala, hija, swala ya maiti,kusoma maulidi, kushona sanda na kadhalika.

- Athari yake ni kuwa, mara baada ya watoto kufikia ngazi hiyo huonekana imetosha na kwamba, wana elimu ya kutosha juu ya uislam. Elimu kuhusu uislam inapungua miongoni mwa waislam.

(b) Uchumi duni kwa wazazi na waalimu.
- Umaskini na kipato kidogo kwa waalimu wa madrasa inakuwa tatizo kubwa kwa uendeshaji wa madrasa zetu. Hali hii husababisha walimu wa madrasa kutenga muda kidogo sana kwa ajili ya kazi ya madrasa na muda kwa ajili ya kujitafutia riziki. Hili hupelekea juhudi za kuboresha madrasa kupungua.
- Vile vile pato la wazazi kuwa dogo huchangia tatizo.
Mara nyingi watu wenye kipato cha chini ndio wanaopeleka watoto wao madrasa, na wenye uwezo na wito wa kiislam wao huwaajiri walimu wa kuwafundisha watoto nyumbani. Kwa sababu hiyo, wazazi wengi hawana uwezo wa kkuchangia fedha muhimu kwa ajili ya madrasa. Wakati mwingine mchango wao huwa kidogo na mgumu kupatikana.

- Athari ya hayo, ni kudorora kwa madrasa zetu na kupatikana kwa watoto, mabarabara, vijana wasio na elimu sahihi ya msingi kuhusu uislam na hatimaye kuporomoka kwa maadili.


(c) Mfumo wa elimu ya nchi na utaratibu wa kisekula.
Mfumo wa elimu ya kisekula umembana kiasi mtoto anayesoma madrasa kutokana na utaratibu ulivyo. Uendeshaji wa elimu ya kisekula umezaa desturi ya “Tuition” (masomo ya ziada), desturi ambayo si tu inamfanya mtoto achoke bali pia inamkosesha muda wa kuhudhuria katika madrasa zetu.

Mfano:
Mtoto wa darasa la kwanza na pili wanaingia shule kwa zamu, mara asubuhi, mara saa tano, mara mchana. Hii inaleta ugumu kwa madrasa kuratibu jinsi ya kuwasaidia watoto.

Mtoto wa darasa la kwanza atokapo shule, anapumzika kidogo, kisha anaenda “Tuition” masomo ya zaida.

Mtoto wa darasa la tano hadi saba, anakosa muda kabisa. Muda wote, kutwa mzima anashughulishwa na elimu ya kisekula na usiku anajisomea nyumbani.

Athari ya tatizo hili ni kushuka kwa mahudhurio ya watoto katika madrasa zetu, na mara nyingine kuwapo kwa mahudhuria yasiyotabirika na kuelezeka. Mara kuna mahudhurio ya kuridhisha mara mabaya.

(d) Shughuli za Kijamii miongoni mwa Waislam.
- Ndani ya jamii ya Kiislam, inapotokea shughuli kama vile harusi na kadhalika, madrasah nyingi kuhusishwa. Mfano kuandaa kaswida kwa ajili ya maulidi harusini. Hili hupunguza muda wa ufundishaji na kujifunza katika madrasa zetu.

- Athari yake ni kuongezeka kwa tatizo katika madrasa zetu. Wazazi wengine huona kua hakuna haja ya watoto kusoma madrasa hizo.

ELIMU YA MADRASSAH TANZANIA:

UTANGULIZI.

Neno la Awali.
Kwa muda mrefu sasa taasisi muhimu ya kiislam, taasisi ya “madrasa” imeachwa na kupoteza hadhi yake. Pamoja na hilo, taasisi hii imeacha pengo kubwa ambalo halizibiki kwa urahisi ila kwa kuinua hadhi ya Madrasa zetu.

Umma wa Waislam unazidi kupata kizazi kinachokosa haki za kimsingi za kuandaliwa kama makhalifa.
Mwenyezi Mungu katika Qurani 51:56 ametueleza “SIKU WAUMBA MAJINI NA WATU ILA WANIABUDU” ili kutekeleza lengo hilo, waislamu lazima waipe hadhi ya Madrasa.
Kadhalika ili kufikia hadhi yetu wanaadam kama inavyoelezwa katika Quran 2:30
waislam lazima tuipe madrasah, hadhi yake sahihi.
Kwa sababu hizo, kuna haja ya kufanya fikra juu ya kuinua hadhi ya madrasa zetu kwa ajili ya kuuendeleza umma wa kiislam utapotea na kuacha wanaoitwa Waislam lakini ummah wa kiislam haupo.

Maana ya Madrasa.
Ilivyozoeleka, madrasa ni kituo cha kiislam ambapo watu hupata elimu juu ya mambo ya msingi katika uislam.
Wengine wameita Shulel za Quran, wengine wamesema, vyuo vya Quran, na wengine wanaelewa kuwa madrasa ni vituo vya watoto ambapo masomo ya Quran, kusoma na kukandika hufundishwa.

Kazi zinazonasibishwa na Taasisi ya Madrasa.
Madrasa zetu Tanzania, kwa muda mrefu tangu Historia ya kuingia kwa uislam nchini zimenasibishwa na kazi zinazofanywa na taasisi hii.
Kwa ujumla madrasa zetu zimejikita katika taaluma zifuatazo:-

(i) Kuandika herufu za kiarabu.
(ii) Kuzisoma herfu za kiarabu.
(iii) Kutafsiri llugha ya kiarabu.
(iv) Kusoma Quran kwa ghaibu au kwa kutazamia.
(v) Jinsi ya kufanya ibada maalum na kanuni zake.
Mfano, ibada, swala, swaum, hija na utoaji zakat na sadakat.

Athari za Madrasa kujikita katika shughuli hizo.

Kwa kuwa Madrasa ni vituo vya elimu ya kiislam, na kwa vile madrasa zinatoa elimu hizo tu, basi elimu ya kiislam inafahamika kuwa ni ile tu inayohusiana na:
- Kusoma na kuandika Quran.
- Kukariri sura za Quran na tafsiri zake.
- Kanuni za utekelezaji wa nguzo tano.
- Kukariri hadithi kadhaa za Mtume (s.a.w).
- Kukariri visa vilivyo katikak lugha ya kiarabu.
Matokeo ya hilo, Uislam nao umeeleweka kukwa ni mambo ya kimaisha yanayohusiana na shughuli hizo tu.
Nje ya shughuli hizo si vitu vya lazima katika uislam.
Mfano kusimamisha dola ya kiislam.

HISTORIA YA ELIMU YA MADRASA TANZANIA KWA UFUPI:

 Historia ya Elimu ya Madrasa Tanzania inanasibiana na Historia ya kuenea kwa uislam katika Afrika Mashariki kuanzia Pwani hadi bara.
 Elimu itolewayo na Madrasa zetu ilichipuka tangu wakati walivyoanza kuja Waarabu kutoka Saudia, Oman, Uajemi, Hadhramaut na Yemen.
 Karne ya 9 na 10 wahamiaji kutoka Saudia walianza kusihi BENADIR (Pwani ya Somalia).
 Karne ya 12 Waarabu wageni (Afro-arabs) walianza kufika hadi mji wa Kilwa.
 Karne ya 12 wageni kutoka Hadhramawt na Yemen waliingia Afrika Mashariki.
Wageni hawa nao pia walitoa elimu inayohusu uislam.
Lakini kufahamu uzito wa elimu waliyoitoa kunategemea ufahamu wa sababu zilizowaleta Afrika Mashariki.
Hawakuja kueneza uislam na kuufundisha uislam.
Bali walikuja kutokana na:-
(i) Njaa iliiyokuwapo Arabuni wakati huo.
(ii) Ukame huko Arabuni.
(iii) Ukandamizaji wa Kisiasa uliotawala huko.

Monday 23 January 2012

Je, Umetanguliza Nini Akhera Ee Ndugu Muislamu?

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ))

((Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Anazo khabari ya mnayoyatenda)) [Al-Hashr: 18]

Siku ya Qiyaamah katika Qur-aan imetajwa kwa majina kadhaa. Baadhi ya Maulamaa wamenukuu kwamba ni majina thelathini na moja takriban.
Miongoni mwayo; Al-Ghad (Kesho), As-Saa'ah (Saa), At-Taghaabun (siku ya hasara au Siku ya kulipizana), Yawmul-Ba'th (Siku ya kufufuliwa), Yawmul-Aakhirah (Siku ya Akhera), Yawmud-Diyn (siku ya malipo), Yawmul-Faswl (siku ya hukumu), Al-Waaqi'ah (tukio), Yawmul-Wa'iyd (siku ya makamio) na kadhalika.


عَنْ جَرِيرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه) قَالَ: كُنَّا عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي صَدْرِ النَّهَارِ فَجَاءَ قَوْمٌ عُرَاةً حُفَاةً مُتَقَلِّدِي السُّيُوفِ عَامَّتُهُمْ مِنْ مُضَرَ, بَلْ كُلُّهُمْ مِنْ مُضَرَ, فَتَغَيَّرَ وَجْهُ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) لِمَا رَأَى بِهِمْ مِنْ الْفَاقَةِ, فَدَخَلَ ثُمَّ خَرَجَ. فَأَمَرَ بِلاَلاً فَأَذَّنَ فَأَقَامَ الصّلاَةَ فَصَلَّى ثُمَّ خَطَبَ فَقَالَ: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالاً كَثِيرًا وَنِسَاءً, وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالأَرْحَامَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا)). و ((اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنْظُرْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ لِغَدٍ)) ))تَصَدَّقَ رَجُلٌ مِنْ دِينَارِهِ مِنْ دِرْهَمِهِ مِنْ ثَوْبِهِ مِنْ صَاعِ بُرِّهِ مِنْ صَاعِ تَمْرِهِ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ)) فَجَاءَ رَجُلٌ مِنْ الأََنْصَارِ بِصُرَّةٍ كَادَتْ كَفُّهُ تَعْجِزُ عَنْهَا, بَلْ قَدْ عَجَزَتْ, ثُمَّ تَتَابَعَ النَّاسُ حَتَّى رَأَيْتُ كَوْمَيْنِ مِنْ طَعَامٍ وَثِيَابٍ حَتَّى رَأَيْتُ وَجْهَ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَتَهَلَّلُ كَأَنَّهُ مُذْهَبَةٌ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((مَنْ سَنَّ فِي الإِِسلاَمِ سُنَّةً حَسَنَةً فَلَهُ أَجْرُهَا وَأَجْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ غَيْرِ أَنْ يَنْقُصَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا, وَمَنْ سَنَّ فِي الإِِسلاَمِ سُنَّةً سَيِّئَةً فَعَلَيْهِ وِزْرُهَا وَوِزْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ غَيْرِ أَنْ يَنْقُصَ مِنْ أَوْزَارِهِمْ شَيْئًا))


Kutoka na Jariyr bin ‘Abdullaah (رضي الله عنه) ambaye amesema :
“Tulikuwa na Mtume (صلى الله عليه وسلم) mapema mchana, wakaja watu ambao walikuwa uchi hawana viatu [walikaribia kuwa uchi kwa mavazi yao ya duni] wakiwa wemebeba mapanga yao. Wengi wao ikiwa si wote walikuwa kutoka [kabila la] Mudhwar.
Uso wa Mtume (صلى الله عليه وسلم) ukabadilika alipoona jinsi gani walivyo maskini [akawa amehuzunika].
Akaingia [nyumbani kwake] kisha akatoka nje na akamuamrisha Bilaal aadhini.
Akaswalisha watu kisha akahutubia akisema: ((Enyi watu, mcheni Allaah Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akaumba kutoka humo mke wake na Akaeneza kutoka wao wawili wanaume wengi na wanawake, na mcheni Ambaye mnamuomba Kwake na jamaa zenu.
Hakika Allaah ni Mwenye kuwaangalieni)) [An-Nisaa:
1] Na ((mcheni Allaah na kila nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho)) [Al-Hashr: 18] ((Atoe mtu sadaka katika dinari zake, nguo zake, ngano au tende zake hata ikiwa ni nusu ya tende moja)).
Akaja mtu kutoka Answaar akaleta furushi ambalo hakuweza hata kulibeba vizuri mkononi, kisha mwengine, kisha mwengine hadi yakawa marundi mawili ya chakula na nguo.
Nikaona uso wa Mtume (صلى الله عليه وسلم) ukinawiri kwa furaha.
Akasema Mtume (صلى الله عليه وسلم):
((Atakayeanza [kutenda] katika Uislamu kitendo chema, atapata thawabu zake na thawabu sawasawa na watakaomfuata bila ya kupunguziwa chochote katika thawabu zao.
Na atakayeanzisha [kutenda] kitendo kiovu atabeba dhambi zake na dhambi za watakaomfuata bila ya kupungiziwa katika dhambi zao chochote)) [Muslim ameisimulia Hadiyth hii kutokana na isnaad ya Shu'bah]

Hivyo jiulize Muislamu, je, umetanguliza nini Akhera? Umetimiza Swalah zako ipasavyo? Umetanguliza Swalah za Sunnah? Umetekeleza Zakaah na Sadaka? Umefunga Ramadhaani na Swawm za Sunnah? Umetekeleza Hajj na 'Umrah? Umesoma Qur-aan kwa wingi na kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake? Umetanguliza wema wa aina yoyote? Umeamrisha mema na kukataza maovu?

Kumbuka kwamba jema lolote utakalolitenda litakuwa ni akiba yako Aakhera na bila shaka utakuja kulikuta na utapata malipo yake siku ya Qiyaamah kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى :

((وَأَقِيمُواْ الصَّلاَةَ وَآتُواْ الزَّكَاةَ وَمَا تُقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللّهِ إِنَّ اللّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ))

((Na shikeni Swalah na toeni Zakah; na kheri mtakazojitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Allaah, hakika Allaah Anayaona mnayoyafanya)) [Al-Baqarah: 110]
Fadhila Za Kusuluhisha Waliogombana:

Fadhila za Kusuluhisha ugomvi ni nyingi, na baada ya kusoma mada kila mmoja wetu anatakiwa akimbiliye kufanya hima kupatanisha ndugu zetu wa Kiislamu waliogombana. Allaah سبحانه وتعالى Amelichukia jambo hili kwani linavunja asili ya undugu wa Kiislamu kama Anavyosema :

((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ))
((Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu)) [Al-Hujuraat: 10]

Na kwa jinsi jambo hili lilivyochukiza hadi kwamba Allaah سبحانه وتعالى Anakataa kupokea amali za watu wanaogombana mpaka wapatane, na hawasamehe watu wao:

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((تُعرض الأعمال في كل أثنين وخميس فيغفر الله لكل أمريء لايشرك بالله شيئاً، إلا إمرءاً بينه وبين أخيه شحناء فيقول: اتركوا هذين حتى يصطلحا)) رواه مسلم

Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba kasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Amali njema (vitendo vyema) hutandazwa kila Jumatatu na Alkhamiys, kisha Allaah Humghufuria kila mtu asiyemshiriki kitu Allaah, isipokuwa mtu aliyekuwa baina yake na baina ya ndugu yake uhasama, Husema: Waacheni hawa wawili mpaka wapatane)) [Muslim]

Kwa hiyo ni hatari kubwa kwa waliogombana kuwa wanapoteza umri wao bure kutenda mema na hali kumbe havipokelewi vitendo hivyo hadi wapatane.


Njia za kupatanisha Watu.
1-Kwanza tia nia kuwa unafanya kupata Radhi na ujira mkubwa kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى, na muombe Allaah سبحانه وتعالى Akuwafikie jambo hili.

2-Msikilize kila mmoja malalamiko yake.

3-Ukishajua sababu ya ugomvi, watajie hatari ya kuhasimikiana kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم .
4-Tafuta wakati na sehemu munaasib kwa wote wawili.

5-Ikibidi kusema uongo, inafaa katika jambo hili kwa kutaka kumridhisha mmojawao ili kuleta suluhisho kama alivyoruhusu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika Hadiythi:

((لَيْسَ الْكَذابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خيرا أو يقول خيرا)) رواه البخاري ومسلم

((Si muongo yule anayesuluhusha watu kwa kusema uongo, kwani anaarifu mema au anasema mema [kwa lengo la kusuluhisha])) [Al-Bukhariy na Muslim]

6-Fanya uadilifu, usipendelee hata kama mmoja ni jamaa yako wa karibu au unampenda zaidi. Amesema Allaah سبحانه وتعالى:

((...فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ))

((…basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Allaah Anawapenda wanaohukumu kwa haki)) [Al-Hujuraat: 9]

Na Anasema tena Allaah سبحانه وتعالى :

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاء لِلّهِ وَلَوْ عَلَى أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْن وَالأَقْرَبِينَ إِِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقَيرًا فَاللّهُ أَوْلَى بِهِمَا فَلاَ تَتَّبِعُواْ الْهَوَى أَن تَعْدِلُواْ وَإِن تَلْوُواْ أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ))

((Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Allaah, ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Allaah anajua vyema mnayoyatenda)) [An-Nisaa: 135]

7-Wakishapatana Inshaa-Llaah omba du'aa Allaah سبحانه وتعالى Awaendeleze masikilizano na mapenzi baina yao na muombe pia Akutakabalie juhudi yako.

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn.
Nani Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)?

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)


(( أَلا إِنَّ أَوْلِيَاء اللّهِ لاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ)) ((الَّذِينَ آمَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ)) لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَياةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ لاَ تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))


((Sikilizeni! Vipenzi vya Allaah hawatakuwa na khofu (siku ya Qiyaamah) wala hawatohuzunika)) ((Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Allaah)) ((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Hapana mabadiliko katika maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu kukubwa)) [Yuunus: 62-64]

Aayah hizi tukufu zinataja 'Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Ni nani basi hao vipenzi Vyake Mola Mtukufu? Je, ndugu Muislamu, unamiliki sifa za kuwa ni waliyyu-Allaah? (kipenzi cha Allaah)?

Vipenzi vya Allaah ni kila aliyekuwa na sifa ya Aayah namba 63 nazo ni kuamini na kuwa na Taqwa, kwa maana kwamba wanafuata waliyoamrishwa na kujiepusha na waliyokatazwa.

Huenda ikawa ni yeyote mmoja wenu madamu tu umetimiza sifa hizo basi umeshakuwa ni 'Walii Wa Allaah', na si kama wanavyodhani watu wengine kuwa ni watu makhsusi kama masharifu na mashekhe wala si watu wa kabila makhsusi au wenye kuvaa nguo makhsusi au kuishi mahali makhsusi [Tarjuma Shaykh 'Abdallaah Swaalih Al-Faarsiy]

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema kuwa hao 'Awliyaa-Allaah' (Vipenzi vya Allaah) hawatokuwa na khofu wala hawatahuzunika.

Kama ilivyosemwa, kwamba huenda wakawa ni waja wowote na sio watu khaswa, wala wasiwe ni Mitume au Mashahidi kama alivyotujulisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):


عن أبي هريرة، رضي الله عنه، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إن من عباد الله عبادا يغبطهم الأنبياء والشهداء)). قيل: من هم يا رسول الله؟ لعلنا نحبهم. قال: ((هم قوم تحابوا في الله من غير أموال ولا أنساب، وجوههم نور على منابر من نور، لا يخافون إذا خاف الناس، ولا يحزنون إذا حزن الناس)). ثم قرأ: (( أَلا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلا هُمْ يَحْزَنُونَ )) الطبري ورواه النسائي ورواه ابن حبان في صحيحه

Imetoka kwa Abu Hurayrah ((Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Miongoni mwa waja wa Allaah, watakuweko wale ambao Mitume na Mashahidi watawadhania kuwa ni wenye bahati)). Akaulizwa "Nani hao ewe Mjumbe wa Allaah ili tuwapende?" Akasema: ((Hawa ni watu waliopendana kwa ajili ya Allaah bila ya sababu ya maslahi ya kifedha au undugu (ujamaa), nyuso zao zitaang'ara katika jukwaa la nuru. Hawatakuwa na khofu (siku hiyo) watakapokuwa na khofu watu wengine, wala hawatahuzunika watakapohuzunika watu wengine)). Kisha akasoma: ((Sikiliezeni! Vipenzi vya Allaah hawatakuwa na khofu (siku ya Qiyaamah) wala hawatohuzunika)) [At-Twabariy, Abu Daawuud, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]

Kisha Anaendelea Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kusema: ((لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَياةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ لاَ تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ)) ((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Hapana mabadiliko katika maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu kukubwa)) [Yuunus: 64]

Maana ya bishara njema katika maisha ya dunia na Aakhirah: عن عبادة بن الصامت؛ أنه قرأ لرسول الله صلى الله عليه وسلم: ( لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ ) ثم قال: فقد عرفنا بشرى الآخرة الجنة، فما بشرى الدنيا؟ قال: (( الرؤيا الصالحة يراها العبد أو تُرَى له، وهي جزء من أربعة وأربعين جزءا أو سبعين جزءا من النبوة)).

'Ubaadah Bin Swaamit alimsomea Mtume ((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah)) kisha akasema:
"Tunajua bishara ya Aakhirah kuwa ni Pepo, lakini nini bishara ya dunia?" Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ni ndoto njema (inayotokea kweli) anayoota mja au anayooteshwa. Ndoto hii ni sehemu moja kutoka sehemu arubaini na nne au sabiini za utume)) [Atw-Twabariy 15:132]

Vile vile imesemwa kuwa bishara njema ni ile anayoletewa Muumini na Malaika wakati wa mauti yake. Humletea bishara njema ya Pepo na maghfirah kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلائِكَةُ أَلا تَخَافُوا وَلا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنْتُمْ تُوعَدُونَ)) (( نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنْفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ)) ((نُزُلا مِنْ غَفُورٍ رَحِيم))

((Hakika waliosema: Mola wetu ni Allaah! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa)) ((Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Aakhirah, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka))
((Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu)) [Fuswswilat: 30-32]

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaalie ni katika Awliyaa Wake. Aamyn.

Sunday 22 January 2012

Hatari Ya Kuihama Qur-aan:

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا))

((Na Mtume amesema: Ee Mola wangu! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur-aan ni kitu kilichohamwa (kilichoachiliwa mbali)))
[Al-Furqaan: 30]

Allaah سبحانه وتعالى Anatuambia jinsi Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Alivyokuwa akilalamika kuwa watu wake wameihama na kuipuuza hii Qur-aan. Makafiri Quraysh walikuwa hawataki kusikiliza Qur-aan, na ilipokuwa ikisomwa walikuwa wakizungumza upuuzi au kuzungumza kwa sauti za juu mazungumzo mengine ili wasiisikie kama Anavyosema Allaah
سبحانه وتعالى :

((وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لاَ تَسْمَعُوا لِهَذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُون))

((Na waliokufuru walisema: Msiisikilize Qur-aan hii, na timueni zogo, huenda mkashinda)) [Fusswilat: 26]

Hali hii ya kuipuuza Qur-aan vile vile iko miongoni mwa Waislamu hali kadhalika, ingawa Waislamu tofauti yake ni kuwa wameiamini na sio kama Makafiri Quraysh ambao ilikuwa ni dhaahiri kuwa waliikanusha na kutoiamini.

Wafasiri Wa Qur-aan wameifafanua Aayah hiyo ya kwanza inayosema,

((إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا))

((Hakika watu wangu wameifanya hii Qur-aan ni kitu kilichohamwa (kilichoachiliwa mbali)))

kwamba: kuihama na kupuuza Qur-aan inawahusu watu wa aina zifuatazo:
1. Wasioisoma kabisa.
2. Wanaoisoma lakini hawajifunzi maana yake.
3. Wanaoisoma na kujifunza maana yake lakini hawafuati maamrisho yake na hawajiepushi na makatazo yake.

Kuihama Qur-aan na kuipuuza ni hatari kubwa kabisa na Mola wetu Mtukufu Ametuonya na Kututisha kupitia Aayah nyingi za Qur-aan.
Miongoni mwa maonyo hayo ni kwamba mja atakuwa na maisha ya dhiki na hufufuliwa siku ya Qiyaamah akiwa kipofu kama ifuatavyo:

((وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى)) ((قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا)) ((قَالَ كَذَلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا وَكَذَلِكَ الْيَوْمَ تُنسَى))

((Na atakayejiepusha na mawaidha Yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Qiyaamah Tutamfufua hali ya kuwa kipofu)) ((Aseme: Ee Mola wangu, mbona Umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?)) (Allaah سبحانه وتعالى) Atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara Zetu, nawe ukazisahau, na kadhaalika leo unasahauliwa)) [Twaaha: 124-126]

Ndugu Waislamu tunaona hatari ya kuipuuza Qur-aan na kuihama basi na tujitahidi kuisoma, kujifunza maana yake na kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake ili tuwe miongoni mwa wale Aliowasifu Allaah سبحانه وتعالى katika hii Qur-aan kuwa wanaisoma 'ipasavyo kusomwa' katika kauli Yake:

((الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلاَوَتِهِ أُوْلَئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ))

((Wale Tuliowapa Kitabu, wakakisoma kama ipasavyo kusomwa, hao ndio kweli wanakiamini)) [Al-Baqarah:121]

Zifuatazo ni kauli za Maswahaba رضي الله عنهم kuhusu 'kuisoma ipasavyo’

Ibn Mas'uud رضي الله عنه: "Naapa kwa Yule Nafsi yangu iko mikononi Mwake, Tilaawa ya kweli ni kufuata yaliohalalishwa na kuacha yaliokatazwa, kusoma kama ilivyoteremshwa, kutokubadilisha maneno katika sehemu zake na kutokuifasiri vingine na ilivyopasa kutafsiriwa" [At-Twabariy 2.567]

Ibn 'Abbaasرضي الله عنهما : "Wenye kuhalalisha yaliyo halali na kukataza yalioharimishwa na hawabadilishi maneno yake".[At-Twabariy 2.567]

'Umar bin Al-Khattwaab رضي الله عنه: "Ni wale ambao inaposomwa Aayah na inapotajwa Rehma wanamuomba Allaah سبحانه وتعالى Rehma Yake, na wanaposoma Aayah inayotaja adhabu, wanajikinga kwa Allaah سبحانه وتعالى nayo". [Al-Qurtubiy 2:95]

Kauli ya 'Umar bin Al-Khattwaab رضي الله عنه: ni kama ilivyokuwa desturi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipokuwa akipita katika Aayah ya Rehma alikuwa akimuomba Allaah سبحانه وتعالى Rehma Yake,
na alipokuwa akisoma Aayah ya adhabu alikuwa akijikinga kwa Allaah سبحانه وتعالى na adhabu.
Maneno yafuatayo ni ya busara ya Mshairi aliyesema kuhusu Qur-aan. Nasi tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atujaalie kuandamana na Kitabu Chake hiki ambacho ndio uongofu wetu kamili na mwangaza utakaotutoa katika kiza na kutuingiza katika Nuru (mwanga), na ndio itakayokuwa sababu ya kufuzu kwetu Duniani na Akhera.

Aamiyn.

Monday 9 January 2012

Utapokea Kitabu Chako Kwa Mkono Gani?

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى): ((وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلاَ كَبِيرَةً إِلاَّ أَحْصَاهَا وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا وَلاَ يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا))

((Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyoogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Hamdhulumu yeyote(( [Al-Kahf: 49].

Aayah hii inatupa picha ya hali itakavyokuwa Siku ya Qiyaamah kwamba matendo yetu yote tutayaona yamerekodiwa katika kitabu. Siku hiyo, ni Siku isiyo na shaka, siku ya miadi, siku ya inayosubiriwa, siku ya majuto, siku ya nyoyo kushituka na macho kukodoka, siku ya mashaka, siku ambayo hakuna budi kwa kila mmoja kuifikia.

Ndugu Waislamu, hii ni siku ya kulipwa mema au mabaya, Siku watakayosimama watu wote na majini mbele ya Mola wa Ulimwengu, siku ambayo kafiri atasema:

((يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا))

((Laiti ningelikuwa udongo!)) [An-Nabaa: 40].

Je, Umefikiria na kuwaza hali yako itakavyokuwa siku hiyo utakaposimama mbele ya Mola wako Mtukufu na huku unasubiri hesabu upewe kitabu chako? Mmoja wetu anapoingia kufanya mtihani au anapokwenda mahakamani kuhukumiwa, moyo wake hudunda kwa nguvu kwa khofu ya kutaka kujua atafanyaje au kuwaza yatakayomkabili. Itakuwaje hali ya moyo siku hiyo wakati matokeo yake yatakuwa ni aidha Pepo ya milele yenye maisha ya raha au moto wenye adhabu kali? Hasa kiwa umeishi umri wako wote katika maasi au umezama katika starehe ya dunia bila kuchuma mema yoyote, vipi itakuwa hali yako siku hiyo?

Amiyrul Muuminiyn amesema manenno ya busara kabisa:
"حاسبوا أنفسكم قبل أن تحاسبوا، وزنوها قبل أن توزنوا، فإن أهون عليكم في الحساب غدًا أن تحاسبوا أنفسكم اليوم، وتزينوا للعرض الأكبر، ((يومئذ تعرضون لا تخفى منكم خافية))

"Hesabuni nafsi zenu kabla ya kuhesabiwa, na zipimeni kabla ya kupimwa, kwani ni bora (wepesi) kwenu kupima (amali zenu) leo kabla ya (kupimwa) kesho kwenye Hesabu, na jipambieni kwa siku ya Hadhara kuu, ((Siku hiyo mtahudhuriwshwa haitafichika siri yoyote))" [Al-Haaqah: 18].

Jipime ndugu Muislamu na jiulize: Je, utakuwa miongoni mwa watakaopewa vitabu vyao mkono wa kulia ukakichukua kwa furaha kubwa na kukionyesha kwa wenzako kama unapopata shahada yako uliyofuzu vizuri sana ukatamani kila mmoja aione, uwaambie kwa furaha 'nimefuzu! nimefuzu vizuri sana! Mfano huo ni kama mfano wa kauli ya Allaah:

((فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَؤُوا كِتَابِيهْ)) ((إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيهْ)) ((فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ)) ((فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ)) ((قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ)) ((كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الأََيَّامِ الْخَالِيَة))

((Basi ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema:
Haya someni kitabu changu!)) ((Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu)) ((Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza)) ((Katika Bustani ya juu)) ((Matunda yake ya karibu)) ((Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita)) [Al-Haaqah: 19-24]

Au utakuwa miongoni mwa wale watakaopewa kitabu chao mkono wa kushoto ukawa na majuto makubwa usiyoyaweza kuyarekebisha tena? Kama Asemavyo Allaah

(سبحانه وتعالى): (( وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيهْ)) ((وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيهْ))

((Na ama atakayepewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingelipewa kitabu changu!)) ((Wala nisingelijua nini hisabu yangu))

Majuto yatazidi kuwa makubwa hadi kwamba mtu atatamani mauti! ((يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ)) ((مَا أَغْنَى عَنِّي مَالِيهْ)) ((هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيهْ))

((Laiti mauti ndiyo yangelikuwa ya kunimaliza kabisa)) ((Mali yangu hayakunifaa kitu)) ((Madaraka yangu yamenipotea))

Wataamrishwa Malaika wamchukue mtu muovu huyo wamtupilie mbali motoni!

((خُذُوهُ فَغُلُّوهُ)) ((ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ)) ((ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ))

(([Pasemwe]: Mshikeni! Mtieni pingu!)) ((Kisha mtupeni Motoni!)) ((Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!))

Sababu ni kwa kuwa:

((إِنَّهُ كَانَ لاَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ))

((Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Allaah Mtukufu)) Hakuamini amri za Allaah (سبحانه وتعالى) na makatazo Yake pamoja na aliyokuja nayo Mtume Wake.

Na pia:

((وَلاَ يَحُضُّ عَلَى طَعَامِ الْمِسْكِينِ))
((Wala hahimizi kulisha masikini))

Ikiwa mtu alishughulishwa duniani na ndugu au jamaa au rafiki, basi Siku hiyo hakuna hata mmoja atakeyemfaa mwenziwe kwani kila mmoja atakuwa analo lake la kukhofia. (( فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ))

((Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu))

Chakula cha humo motoni ni usaha unaotoka katika miili ya watu na mti wa Zakkuum ulio mchungu ajabu, ulio na miba na unaokirihisha kabisa! ((وَلاَ طَعَامٌ إِلاَّ مِنْ غِسْلِينٍ)) (( لاَ يَأْكُلُهُ إِلاَّ الْخَاطِؤُونَ))

((Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni)) ((Chakula hicho hawakili ila wakosefu)) [Al-Haaqah: 25-37].

Nani atakayeridhika kuwa katika hali hiyo? Kwanini basi mtu aache kuswali, kufunga Swawm na kutenda mema? Au kupoteza wakati kwa mambo ya upuuzi? Au kumuasi Mola Mtukufu na hali siku ya Qiyaamah mtu atasimama mbele Yake kujibu kila baya alilolitenda.

Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Hadiythil-Qudsiyy

((ياعبادي إنما هي أعمالكم أحصيها لكم فمن وجد خيراً فليحمد الله ومن وجد غير ذلك فلا يلومن إلا نفسه)) مسلم

((Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu Ninavyovihesabu, kwa ajili yenu Nikakulipeni. Kwa hivyo anayekuta wema amshukuru Allaah na yule anayekuta yasiokuwa mema (basi) ajilaumu mwenyewe)) [Muslim].

Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atujaalie miongoni mwa watakaopokea vitabu vyao kuliani kama Anavyosema:

((فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ)) ((فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا )) ((وَيَنقَلِبُ إِلَى أَهْلِهِ مَسْرُورًا))

((Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia)) ((Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi)) ((Na arudi kwa ahli zake na furaha)) [Al-Inshiqaaq: 7-9].

Na Asitujaalie tukawa miongoni mwa wale watakaopewa vitabu vyao katika mkono wa kushoto au nyuma ya migongo yao:

((وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاء ظَهْرِهِ)) ((فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا )) ((وَيَصْلَى سَعِيرًا))

((Na ama atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake)) ((Basi huyo ataomba kuteketea)) ((Na ataingia Motoni)) [Al-Inshiqaaq: 10-12]

Tuesday 3 January 2012

Vitumbua Vya Shira

* Vitafunio




Vipimo

1. Unga

2. gilasi

3. Mayai

4. Hamira

vijiko vya chai

Maziwa ya maji 2 gilasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Weka mayai katika bakuli kisha yapige vizuri.

2. Tia maziwa koroga.

3. Tia hamira, koroga.

4. Tia unga uchanganye vizuri.

5. Weka uumuke, ukiwa tayari choma/pika kama unavyopika vitumbua vya kawaida.

6. Vikishapoa weka kwenye sinia na mimina shira vikiwa tayari kuliwa.
Shira:

Sukari

1. gilasi

Maji

2. gilasi

ladha - hiliki au arki (rose flavour) n.k 5 matone.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika.

1. Weka vitu vyote pamoja katika sufuria uweke motoni ichemke kidogokidogo hadi iwe tayari. Isiwe nzito, bali nyepesi.

2. Tia ladha, iache ipowe na kuwa tayari kumiminwa juu ya vitumbua.