Wednesday 3 October 2012

VITA VYA majimaji “MACHINJIO” YA WAISLAMU


Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge,hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji.

Jambo kubwa la mahala hapo ni Kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na….
walizikwa kwa pomoja.Na kando ya kaburi hilo la pomoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwa mwaka 2007.

Baada ya kusaini kitabu cha wageni,na kulipa ada ya kituo,muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo.

ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa mwislam jambo moja litakustuwa.Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni waislaam .

linaanza jina lake la kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman[Dominic]Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya majimaji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya kikristo na baadae kunyongwa,wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru,wote katika hao walionyongwa walikuwa ni waislam.

Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya Yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake[huyo padri] aliiyaandika hayo majina.

Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo.Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona wakubwa wa kituo hicho.

Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009.nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo,iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya majimaji,haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya majimaji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu,jina la padri,sahihi yake na wadhifa wake katika kanisa katoliki pia vimeondolewa,na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza Muhudumu kulikoni? Akasema……. Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya Tanu na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M.S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na mzungu wa kijerumani.

Binti huyu na na mumewe wa kijerumani walikuja hapa Songea matembezi.

Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha.

Hivyo ndio karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni waislaam,wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano.

Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa pia peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa,unaanza kuona picha za mashujaa wa majimaji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija.

kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani.Chini ya kila picha kuna jina la mwenye picha.Katika picha hizo majina Ukipanda gorofani utaona silaha za kijadi,mikuki,pinde,mishale,ngao,n.k.

Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita.mavazi ya vita ya askari wa majimaji wengi walivaa kanzu za kiislaam na vilemba.

Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika”Rosary”[hili ni jina la kikristo,hasa la kikatoliki,ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba]lakini unapotazama hicho kilichoitwa “Rosary” utaona si Rosary, bali ni Tasbihi hasa ya kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake,33,33,34.maneno yaliyoandikwa kuelezea Rosary hizo ambazo ni Tasbihi ni “Hizi ni Rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.

ukweli ni kwamba hawa askari wa majimaji wengi walikuwa ni waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia Tasbihi hizo kufanya Dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani.

Midhali sisi waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama waislaam,wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka.

Hapo gorofani kuna jingine la kasisimua.kuna makopo au magudulia.

Wameandika kuwa,haya ndio makopo ambayo askari wa majimaji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani[kushika udhu na sio kunawa]pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga na Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za uhakika ziko Jimbo kuu la Wakatoliki,Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.Tulitakiwa tupate kibari cha Askofu mkuu.Hatukukipata.

Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia tulijifunza mambo yafuatayo:-

1.Vita vya majimaji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao.La!!!Vilikuwa ni vita vya waislaam wakipigana na wakristo wa kijerumani waliovamia maeneo asilia ya waislaam kwa lengo la kuuwa uislaam na kusimamisha Kanisa.kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya majimaji ni mazingira ya kiislaam,kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa kijerumani ila katika miji ya waislaam.Kilwa.Bagamoyo.n.k.kwa nini wauliwe maeneo ya waislaam tu?walifuata nini huko?

2.kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya majimaji.Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa kijerumani,wakati ukweli si hivyo.Ukweli ni kwamba vita vya majimaji vilikuwa ni vita baina ya waislaam na wakrito wa kijerumani,waafrika wakristo wa songea walijiunga na wakristo wenzao wa kijerumani dhidi ya waafrika wenzao wa kiislaam.

3.Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao. MWISHO Kuna haja ya wasomi wetu wa kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa Historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri.Taasisi za kiislaam na watu binafsi[matajiri]wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.

Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa kisiwani ,huko nikamkuta mzungu wa kifaransa akiandika historia ya kilwa kisiwani akiitwaThiery,ameweka kambi na majenereta ya umeme,solar power,na makompyuta.kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni Misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale.

Kilwa kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za kiislaam katika mwambao wa Afrika mashariki,ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah.

Tuliposoma kazi ile ya Yule Thiery mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa.sikuwa na la kumfanya.Kizazi cha vijana wa kiislaam hakitopata historia ya kweli ya kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike,na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika uislam wao.