JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu unajisi wa mbwa wa kufuga.
Mbwa
mwenyewe hawezi kusemwa ni najisi kwa kutokuwa na dalili ya hilo,
isipokuwa mate yake na majimaji ya puani mwake yanachukuliwa ni najisi
kishari’ah ikiwa ni wa kufuga au vinginevyo kwa dalili iliyopatikana
kutoka katika Hadiyth. Na kwa hivyo chombo chochote ambacho kitarambwa
na mbwa kinapaswa kutwaharishwa kwa kuoshwa mara saba bila kutofautisha
ni mbwa gani aliyekiramba, mojawapo kwa mchanga. Abu Hurayrah (Radhiya
Allaahu ‘anhu) amesema, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) amesema: “Kukitwahirisha chombo kilichorambwa na mbwa kunafanywa kwa kuosha mara saba, mojawapo kwa udongo” (Ahmad, Muslim, Abu Daawuud na al-Bayhaqiy).
Na
ikiwa ataramba chombo chenye chakula kikavu, kile chakula kilichoguswa
na mdomo wa mbwa na kilicho pembezoni mwake kinatakiwa kitupwe, ama
kilichobaki ni twahara kinaweza kubakishwa. Ama manyoya ya mbwa yakiwa
makavu ni twahara. Sehemu iliyo najisi ya mbwa ni ule mdomo wake kwa
ajili ya umandemande.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
No comments:
Post a Comment