(f) NJIA ZA KUFUNDISHIA QUR-AN KWENYE MADRASA ZETU:
Njia na mbinu pamoja na mikakati mbali mbali ni muhimu sana katika ufundishaji wa usomaji Quran katika madras zetu, vinginevyo mtoto atasoma muda mrefu sana ili kuelewa. Baadhi ya mbinu za kufundishia ni pamoja na kusoma herufi bila irabu kwa njia ya ubao, kadi, daftari n.k.
MUHIMU:
- Mwalimu afundishe kwanza herufi bila irabu. Yaani: ALIF, BE …….
- Kisha afundishe Irabu. Yaani: FAT’HA, KISRA, ……
- Afundishe kuchanganya herufi hizo pamoja na irabu zake;
Mfano: BE FAT’HABA, TE FAT’HATA …….
- Mwalimu atumie michezo kadhaa kwa watoto kuzitambua herufi.
Mfano: NGAZINGAZI, KIKAPU, UPANGAJI, GURUDUMU ZA GARI, NYUMBA …. n.k.
- Mwalimu afundishe kuchanganya SILABI ili kupata neno. Ni vizuri Mwalimu akaanza na kinachoeleweka kwenda kisichoeleweka.
Mfano: Kumwezesha motto kuandika BABA kwa herufi za Kiarabu, kasha aandike neno la kiarabu kwa herfu hizo.
HITIMISHO
Mwalimu anapaswa kujua anachokifundisha, pia kufahamu na kuweza kutumia njia na mbinu muafaka. Kwa kawaida hatupaswi kulenga kusema sana, au kueleza mengi, bali tulenge kuwezesha mengi kufahamika kwa urahisi zaidi.
Kwa muda mrefu MADRASA zimesahaulika na kusababisha athari mbaya.
Ili kuziendeleza tunapaswa kuzingatia kazi zinazotakiwa kufanywa na madrasa na zipi zinafanywa. Kuelewa tatizo kwa undani. Historia ya Madrasa Tanzania ni muhimu kufahamika ili kurudisha mzizi wa tatizo. Kadhalika, Matatizo yanayoikabili taasisi ya Madrasa na ufumbuzi wake ni muhimu vikajadiliwa.
Aidha , kuna haja ya kukumbuka taluma muhimu kwa walimu wa Madrasa na kuona kama wengi wanazo.
Kama si hivyo, basi mikakati iwepo kuwawezesha walimu wa Madrasa kuendesha madrasa zetu (Uendeshaji Madrasa) pamoja na kuwa na mbinu bora za kufundishia katika madrasah zetu.
No comments:
Post a Comment