ELIMU YA MADRASSAH TANZANIA:
UTANGULIZI.
Neno la Awali.
Kwa muda mrefu sasa taasisi muhimu ya kiislam, taasisi ya “madrasa” imeachwa na kupoteza hadhi yake. Pamoja na hilo, taasisi hii imeacha pengo kubwa ambalo halizibiki kwa urahisi ila kwa kuinua hadhi ya Madrasa zetu.
Umma wa Waislam unazidi kupata kizazi kinachokosa haki za kimsingi za kuandaliwa kama makhalifa.
Mwenyezi Mungu katika Qurani 51:56 ametueleza “SIKU WAUMBA MAJINI NA WATU ILA WANIABUDU” ili kutekeleza lengo hilo, waislamu lazima waipe hadhi ya Madrasa.
Kadhalika ili kufikia hadhi yetu wanaadam kama inavyoelezwa katika Quran 2:30
waislam lazima tuipe madrasah, hadhi yake sahihi.
Kwa sababu hizo, kuna haja ya kufanya fikra juu ya kuinua hadhi ya madrasa zetu kwa ajili ya kuuendeleza umma wa kiislam utapotea na kuacha wanaoitwa Waislam lakini ummah wa kiislam haupo.
Maana ya Madrasa.
Ilivyozoeleka, madrasa ni kituo cha kiislam ambapo watu hupata elimu juu ya mambo ya msingi katika uislam.
Wengine wameita Shulel za Quran, wengine wamesema, vyuo vya Quran, na wengine wanaelewa kuwa madrasa ni vituo vya watoto ambapo masomo ya Quran, kusoma na kukandika hufundishwa.
Kazi zinazonasibishwa na Taasisi ya Madrasa.
Madrasa zetu Tanzania, kwa muda mrefu tangu Historia ya kuingia kwa uislam nchini zimenasibishwa na kazi zinazofanywa na taasisi hii.
Kwa ujumla madrasa zetu zimejikita katika taaluma zifuatazo:-
(i) Kuandika herufu za kiarabu.
(ii) Kuzisoma herfu za kiarabu.
(iii) Kutafsiri llugha ya kiarabu.
(iv) Kusoma Quran kwa ghaibu au kwa kutazamia.
(v) Jinsi ya kufanya ibada maalum na kanuni zake.
Mfano, ibada, swala, swaum, hija na utoaji zakat na sadakat.
Athari za Madrasa kujikita katika shughuli hizo.
Kwa kuwa Madrasa ni vituo vya elimu ya kiislam, na kwa vile madrasa zinatoa elimu hizo tu, basi elimu ya kiislam inafahamika kuwa ni ile tu inayohusiana na:
- Kusoma na kuandika Quran.
- Kukariri sura za Quran na tafsiri zake.
- Kanuni za utekelezaji wa nguzo tano.
- Kukariri hadithi kadhaa za Mtume (s.a.w).
- Kukariri visa vilivyo katikak lugha ya kiarabu.
Matokeo ya hilo, Uislam nao umeeleweka kukwa ni mambo ya kimaisha yanayohusiana na shughuli hizo tu.
Nje ya shughuli hizo si vitu vya lazima katika uislam.
Mfano kusimamisha dola ya kiislam.
HISTORIA YA ELIMU YA MADRASA TANZANIA KWA UFUPI:
Historia ya Elimu ya Madrasa Tanzania inanasibiana na Historia ya kuenea kwa uislam katika Afrika Mashariki kuanzia Pwani hadi bara.
Elimu itolewayo na Madrasa zetu ilichipuka tangu wakati walivyoanza kuja Waarabu kutoka Saudia, Oman, Uajemi, Hadhramaut na Yemen.
Karne ya 9 na 10 wahamiaji kutoka Saudia walianza kusihi BENADIR (Pwani ya Somalia).
Karne ya 12 Waarabu wageni (Afro-arabs) walianza kufika hadi mji wa Kilwa.
Karne ya 12 wageni kutoka Hadhramawt na Yemen waliingia Afrika Mashariki.
Wageni hawa nao pia walitoa elimu inayohusu uislam.
Lakini kufahamu uzito wa elimu waliyoitoa kunategemea ufahamu wa sababu zilizowaleta Afrika Mashariki.
Hawakuja kueneza uislam na kuufundisha uislam.
Bali walikuja kutokana na:-
(i) Njaa iliiyokuwapo Arabuni wakati huo.
(ii) Ukame huko Arabuni.
(iii) Ukandamizaji wa Kisiasa uliotawala huko.
No comments:
Post a Comment