Vitumbua Vya Shira
* Vitafunio
Vipimo
1. Unga
2. gilasi
3. Mayai
4. Hamira
vijiko vya chai
Maziwa ya maji 2 gilasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Weka mayai katika bakuli kisha yapige vizuri.
2. Tia maziwa koroga.
3. Tia hamira, koroga.
4. Tia unga uchanganye vizuri.
5. Weka uumuke, ukiwa tayari choma/pika kama unavyopika vitumbua vya kawaida.
6. Vikishapoa weka kwenye sinia na mimina shira vikiwa tayari kuliwa.
Shira:
Sukari
1. gilasi
Maji
2. gilasi
ladha - hiliki au arki (rose flavour) n.k 5 matone.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika.
1. Weka vitu vyote pamoja katika sufuria uweke motoni ichemke kidogokidogo hadi iwe tayari. Isiwe nzito, bali nyepesi.
2. Tia ladha, iache ipowe na kuwa tayari kumiminwa juu ya vitumbua.
No comments:
Post a Comment