Monday, 30 January 2012

MBINU ZA KUFUNDISHIA (DARASA LA KWANZA).
KUTAMBUA, KUANDIKA NA KUSOMA HERUFI ZA QUR-ANI:

• Mwalimu awaonyeshe na kuwatamkia wanafunzi herufi mojamoja Atumie picha na kadi.
• Wanafunzi wamfuatishe Mwalimu kutamka herufi moja moja kwa wote kisha mmoja mmoja.
• Wanafunzi wafanye mazoezi ya kuandika herufi moja moja katika ardhi, ubaoni, katika karatasi ngumu, n.k.
• Mwalimu awatambulishe wanafunzi hatua kwa hatua alama za Irabu, tanwin na sakna na atoe mazoezi ya kutosha ya kusoma na kuandika herufi za Kiarabu zikiwa na alama hizo.
• Mwalimu awaonyeshe herufi moja moja inavyokuwa ikiwa inaungwa mwanzoni, katikati na mwishoni mwa neno. Abainishe herufi zisizoungika na atoe mazoezi ya kutosha ya kusoma na kuandika.
• Mwalimu awatambulishe wanafunzi alama za madda na shadda na zinavyotumika katika kusoma•
• Mwalimu atoe mazoezi mengi ya kusoma na kuandika.

LENGO (MWANAFUNZI)Aweze kusoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu.

VIFAA/REJEA.
• Ubao na chaki.
• Kadi za herufi.
• Kadi za maneno.
• Mbao/ubao.
• Juzuu Amma.
• Kitabu cha I (IPC).

No comments:

Post a Comment