Nani Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)?
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
(( أَلا إِنَّ أَوْلِيَاء اللّهِ لاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ)) ((الَّذِينَ آمَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ)) لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَياةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ لاَ تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))
((Sikilizeni! Vipenzi vya Allaah hawatakuwa na khofu (siku ya Qiyaamah) wala hawatohuzunika)) ((Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Allaah)) ((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Hapana mabadiliko katika maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu kukubwa)) [Yuunus: 62-64]
Aayah hizi tukufu zinataja 'Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Ni nani basi hao vipenzi Vyake Mola Mtukufu? Je, ndugu Muislamu, unamiliki sifa za kuwa ni waliyyu-Allaah? (kipenzi cha Allaah)?
Vipenzi vya Allaah ni kila aliyekuwa na sifa ya Aayah namba 63 nazo ni kuamini na kuwa na Taqwa, kwa maana kwamba wanafuata waliyoamrishwa na kujiepusha na waliyokatazwa.
Huenda ikawa ni yeyote mmoja wenu madamu tu umetimiza sifa hizo basi umeshakuwa ni 'Walii Wa Allaah', na si kama wanavyodhani watu wengine kuwa ni watu makhsusi kama masharifu na mashekhe wala si watu wa kabila makhsusi au wenye kuvaa nguo makhsusi au kuishi mahali makhsusi [Tarjuma Shaykh 'Abdallaah Swaalih Al-Faarsiy]
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema kuwa hao 'Awliyaa-Allaah' (Vipenzi vya Allaah) hawatokuwa na khofu wala hawatahuzunika.
Kama ilivyosemwa, kwamba huenda wakawa ni waja wowote na sio watu khaswa, wala wasiwe ni Mitume au Mashahidi kama alivyotujulisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عن أبي هريرة، رضي الله عنه، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إن من عباد الله عبادا يغبطهم الأنبياء والشهداء)). قيل: من هم يا رسول الله؟ لعلنا نحبهم. قال: ((هم قوم تحابوا في الله من غير أموال ولا أنساب، وجوههم نور على منابر من نور، لا يخافون إذا خاف الناس، ولا يحزنون إذا حزن الناس)). ثم قرأ: (( أَلا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلا هُمْ يَحْزَنُونَ )) الطبري ورواه النسائي ورواه ابن حبان في صحيحه
Imetoka kwa Abu Hurayrah ((Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Miongoni mwa waja wa Allaah, watakuweko wale ambao Mitume na Mashahidi watawadhania kuwa ni wenye bahati)). Akaulizwa "Nani hao ewe Mjumbe wa Allaah ili tuwapende?" Akasema: ((Hawa ni watu waliopendana kwa ajili ya Allaah bila ya sababu ya maslahi ya kifedha au undugu (ujamaa), nyuso zao zitaang'ara katika jukwaa la nuru. Hawatakuwa na khofu (siku hiyo) watakapokuwa na khofu watu wengine, wala hawatahuzunika watakapohuzunika watu wengine)). Kisha akasoma: ((Sikiliezeni! Vipenzi vya Allaah hawatakuwa na khofu (siku ya Qiyaamah) wala hawatohuzunika)) [At-Twabariy, Abu Daawuud, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]
Kisha Anaendelea Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kusema:
((لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَياةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ لاَ تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))
((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Hapana mabadiliko katika maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu kukubwa)) [Yuunus: 64]
Maana ya bishara njema katika maisha ya dunia na Aakhirah:
عن عبادة بن الصامت؛ أنه قرأ لرسول الله صلى الله عليه وسلم: ( لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ ) ثم قال: فقد عرفنا بشرى الآخرة الجنة، فما بشرى الدنيا؟ قال: (( الرؤيا الصالحة يراها العبد أو تُرَى له، وهي جزء من أربعة وأربعين جزءا أو سبعين جزءا من النبوة)).
'Ubaadah Bin Swaamit alimsomea Mtume ((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah)) kisha akasema:
"Tunajua bishara ya Aakhirah kuwa ni Pepo, lakini nini bishara ya dunia?" Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ni ndoto njema (inayotokea kweli) anayoota mja au anayooteshwa. Ndoto hii ni sehemu moja kutoka sehemu arubaini na nne au sabiini za utume)) [Atw-Twabariy 15:132]
Vile vile imesemwa kuwa bishara njema ni ile anayoletewa Muumini na Malaika wakati wa mauti yake. Humletea bishara njema ya Pepo na maghfirah kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلائِكَةُ أَلا تَخَافُوا وَلا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنْتُمْ تُوعَدُونَ))
(( نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنْفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ))
((نُزُلا مِنْ غَفُورٍ رَحِيم))
((Hakika waliosema: Mola wetu ni Allaah! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa))
((Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Aakhirah, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka))
((Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu)) [Fuswswilat: 30-32]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaalie ni katika Awliyaa Wake. Aamyn.
No comments:
Post a Comment