Kustawi kwa Elimu ya Madrasa Afrika Mashariki:
Mwaka 1332, Mwarabu aitwaye IBN BATUTA alipotembelea Kilwa alikuta mji umekaliwa na waliokuwa wakitumia lugha ya Kiswahili.
Baadaye miji ya Tanga, Dar-es-Salaam, Mombasa, Lamu, Malindi, na Mikindani vikawa vituo vya kueneza uislam na elimu ya kiislam katika miji ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Zaire, Msumbiji, Malawi na Burundi.
Maarifa yaliyotolewa na njia za kufundishia.
Maarifa yaliyotolewa na kuonekana hayo ndiyo maarifa ya uislam ni pamoja na:
(i) Zipi ni nguzo za imani na maana yake.
(ii) Zipi nguzo za Swala na maana yake.
(iii) Namna ya kusoma Quran, lugha ya kiarabu na vira kadhaa.
(iv) Sirah ya Mtume (s.a.w)
(v) Kanuni zinazotawala utendaji wa Ibada Maalumu.
Maarifa haya yalifundishwa kwa njia kuu ya Kipurure,(yaani Mwanafunzi hakusoma kwa njia ya kuuliza na kudadisi.
Walimu wa kufundisha hayo, ni wale tu, walioonekana wanaweza kuyasoma hayo. Hakukuwa na mazingatio kuhusu uwezo na ujuzi wa mfundishaji kufikisha maarifa anayoyatoa.
Kwa sababu hizo, pia njia kuu ya kudhibiti nidhamu, ilibaki kuwa ni viboko tu.
Kwa ujumla taaluma kuu za elimu ya Madrasa zilizotawala ni KUSOMA, KUANDIKA, KUIFADHI na KUIGA ambazo zilitolewa na walioweza kuzipata taaluma hizo.
Dosari za Elimu ya Madrasa iliyotolewa wakati wa Waarabu.
Dosari hizo zimetokana na asili ya kuenea kwa dini na elimu ya Kiislam Afrika Mashariki, hususan Tanzania.
Tatizo linakuja kwa vile Uislam na elimu ya Kiisam:-
(i) Vilenea katika taratibu za walioeneza kujitafutia maisha yao wala si kwa madhumini ya kufanya umisionari.
(ii) Vilienezwa na waislam ambapo hawakuwa na maandilizi ya kufanya hivyo, hivyo hakukuwa na matayarisho yoyote ya malengo ya kielimu.
Matokeo yake uislam ulifundishwa ili kupata wenzi na washirika katika masuala ya kijamii kama vile:
o Misiba
o Harusi n.k..
(i) Zilifundishwa Taaluma chache tu.
Mfano: Kusoma, Kuandika, Kukariri Quran.
Taaluma hizo si pana kiasi cha kuwawezesha wanafunzi kuuhami uislam kifikra au vyovyote, taaluma hizo hazimwezeshi mwanafunzi kumudu changamoto zinazoibuka kila kukicha; Japo uislam haushindwi na changamoto yoyote ile.
(ii) Njia za kuendeleza nidhamu, na maadili zilikuwa ni viboko tu, ukali tu, pasi na kuchunguza tatizo kwa lengo la kuondoa tatizo hilo na kusaidia.
(iii) Njia za kufundishia hazikuzingatia umuhimu wa kuendeleza na kuhusisha nyanja tatu za kujifunza.
(a) Nyanja ya ung’amuzi (Cognitive domain).
(b) Nyanja ya matendo (Psychomotor domain)
(c) Nyanja ya kuhusisha (Affective domain)
Kila nyanza hapo inaumuhimu katika uislam wa mtu mmoja mmoja au jamii na hatimaye Ummah.
(iv) Hakukuwapo chombo maalum cha kijamii, kinachosimamia swala zima la utoaji wa Elimu hii. Matokeo yake kila mmoja alifundisha kadiri na namna alivyodhani ni sawa.
Athari za dosari hizo
(i) Kukosekana kwa taaluma muhimu za kifiqih
Mfano:
- Taaluma inayowezesha kuhusianisha mazingira na fatwa kadhaa za kifiqih.
- Taaluma inayofafanua hukumu kadhaa za kifiqih na yanayotokea katika maisha.
Katika hili, kumekosekana taaluma ya kubainisha tofauti ya RIRA na HIBA.
(ii) Watu wachache sana ndio waliweza kuendelea na elimu ya Madrasa kwa
kiwango cha juu kwa kulinganisha na waislam wengine.
Mfano:-
Ni Masheikh wachache waliweza kufikia kiwango fulani. Matokeo yake hata vitu vidogo vidogo kuweza kufahamika kwa waislam wote, vinafahamika na masheikh tu.
(iii) Kuibuka kwa Matabaka miongoni mwa waislam kutokana na dosari hizo,
kumeibuka matabaka kadhaa mingoni mwa waislam.
Mfano:
o Tabaka la wasomi wa elimu katika mfumo huu wa madrasa tu.
o Tabaka la waliosoma elimu ya madrasa kidogo na elimu ya kisekula kidogo.
o Tabaka la waliosoma kiasi elimu ya kisekula na kukosa elimu ya madrasa lakini badaye (ukubwani) wakajifunza elimu ya uislam kwa mfumo mwingine.
Mahusiano ya matabaka haya hayasaidii kuendeleza uislam na waislam kwa ujumla, ni sumu kwa maendeleo ya jamii ya kiislam.
MATATIZO YANAYOIKABILI ELIMU YA MADRASA TANZANIA:
Taasisi ya Madrasah inazidi kupoteza hata hadhi yake ndogo iliyokuwa nayo.
Mfano:
Jamii haiipi hata thamani inayostahiki licha ya kuwa madrasa ni taasisi muhimu katika kurithisha mila, destuli na mfumo mzima wa uislam toka kizazi hadi kingine. Wazazi na watoto wa kiislam leo hii hawana hari ya kupeleka watoto wao kwenye vituo vya madrasa. Wala wazazi hao hawana hata haja ya kujua mikati ya madrasa zinazowazunguka.
(ii) Matatizo.
Matatizo yanayoikabili elimu ya madrasa ni:
Matatizo ya Kitaasisi (Institutional Problems.
)
(a) Hakuna mfumo wa uendeshaji elimu ya madrasa.
Mfumo huo hautoi picha halisi juu ya nani hasa ndiye mratibu au msimamizi wa elimu ya Madrasa. Kwa sababu hiyo hakuna upimaji wala tathimini yoyote ili kuelewa kuwa nani anastahiki kuwa msimizi wa elimu hii muhimu.
(b) Kukosekana kwa “usare” (uniformity) katika ufundisjaji.
Matokeo yake anapohama mtoto kwenda madrasa nyingine anaathirika kitaaluma.
(c) Hakuna utaratibu fasaha/muafaka wa kuwahusisha wazazi wa Kiislam katika kujadili maendeleo na kutathimini uendeshaji wa madrasa. Athari yake ni wazazi kutojihusisha na uendelezaji wa madrasa zetu na ufuatiliaji wa taaluma muhimu zipatikanazo.
(d) Kukosekana kwa utaratibu wa kubadilishana mawazo baina ya waalimu tofauti tofauti, juu ya uboreshaji wa njia za ufundishaji na mafanikio katika uendeshaji madrasa.
(e) Kukosekana kwa mipango inayohusiana na madrasa, wanafunzi na walimu. Athari yake ni kupungua kwa idadi ya wanafunzi na walimu wa madrasa.
(f) Kukosekana kwa utaratibu maalumu juu ya vigezo vinavyomuwezesha mtu kuwa mwalimu.
Kwa kawaida yeyote anayejua kusoma na kuandika herufi za kiarabu, kusoma Quran na mambo kadhaa katika Ibada maalumu za kifiqih, aweza kuwa mwalimu hata kama sifa za kitabia, na uwezo wa kurithisha elimu kwake ni vikwazo.
TANBIH:
Aina za walimu zaweza kuwa kama ifuatavyo:-
(i) Mwenye sifa (Qualified) – Anazo sifa kitabia, anaweza kuwa na ujuzi wa kufundisha na ana elimu.
(ii) Mwenye sifa (Underqualified) – Anayo elimu ila hana mbinu bora za ufundishaji.
(iii) Asiye na sifa (Unqualified) – Hana sifa hata kidogo. Huyu ni hatari sana.
Matatizo ya Kijamii.
(a) Fikra za watu juu ya elimu ya madrasa na thamani yake
- Jamii na mtu mmoja mmoja wanachukulia elimu ya msingi ya madrasa ni kusoma Quran na kujua kanuni muhimu za utekelezaji wa Ibada maalumu kama vile Swala, hija, swala ya maiti,kusoma maulidi, kushona sanda na kadhalika.
- Athari yake ni kuwa, mara baada ya watoto kufikia ngazi hiyo huonekana imetosha na kwamba, wana elimu ya kutosha juu ya uislam. Elimu kuhusu uislam inapungua miongoni mwa waislam.
(b) Uchumi duni kwa wazazi na waalimu.
- Umaskini na kipato kidogo kwa waalimu wa madrasa inakuwa tatizo kubwa kwa uendeshaji wa madrasa zetu. Hali hii husababisha walimu wa madrasa kutenga muda kidogo sana kwa ajili ya kazi ya madrasa na muda kwa ajili ya kujitafutia riziki. Hili hupelekea juhudi za kuboresha madrasa kupungua.
- Vile vile pato la wazazi kuwa dogo huchangia tatizo.
Mara nyingi watu wenye kipato cha chini ndio wanaopeleka watoto wao madrasa, na wenye uwezo na wito wa kiislam wao huwaajiri walimu wa kuwafundisha watoto nyumbani. Kwa sababu hiyo, wazazi wengi hawana uwezo wa kkuchangia fedha muhimu kwa ajili ya madrasa. Wakati mwingine mchango wao huwa kidogo na mgumu kupatikana.
- Athari ya hayo, ni kudorora kwa madrasa zetu na kupatikana kwa watoto, mabarabara, vijana wasio na elimu sahihi ya msingi kuhusu uislam na hatimaye kuporomoka kwa maadili.
(c) Mfumo wa elimu ya nchi na utaratibu wa kisekula.
Mfumo wa elimu ya kisekula umembana kiasi mtoto anayesoma madrasa kutokana na utaratibu ulivyo. Uendeshaji wa elimu ya kisekula umezaa desturi ya “Tuition” (masomo ya ziada), desturi ambayo si tu inamfanya mtoto achoke bali pia inamkosesha muda wa kuhudhuria katika madrasa zetu.
Mfano:
Mtoto wa darasa la kwanza na pili wanaingia shule kwa zamu, mara asubuhi, mara saa tano, mara mchana. Hii inaleta ugumu kwa madrasa kuratibu jinsi ya kuwasaidia watoto.
Mtoto wa darasa la kwanza atokapo shule, anapumzika kidogo, kisha anaenda “Tuition” masomo ya zaida.
Mtoto wa darasa la tano hadi saba, anakosa muda kabisa. Muda wote, kutwa mzima anashughulishwa na elimu ya kisekula na usiku anajisomea nyumbani.
Athari ya tatizo hili ni kushuka kwa mahudhurio ya watoto katika madrasa zetu, na mara nyingine kuwapo kwa mahudhuria yasiyotabirika na kuelezeka. Mara kuna mahudhurio ya kuridhisha mara mabaya.
(d) Shughuli za Kijamii miongoni mwa Waislam.
- Ndani ya jamii ya Kiislam, inapotokea shughuli kama vile harusi na kadhalika, madrasah nyingi kuhusishwa. Mfano kuandaa kaswida kwa ajili ya maulidi harusini. Hili hupunguza muda wa ufundishaji na kujifunza katika madrasa zetu.
- Athari yake ni kuongezeka kwa tatizo katika madrasa zetu. Wazazi wengine huona kua hakuna haja ya watoto kusoma madrasa hizo.
No comments:
Post a Comment