Monday, 30 January 2012

SOMO LA FIQH (DARASA LA KWANZA):

Najsi na namna ya kujitwaha-risha.
• Vitu vilivyonajisi.
• Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
• Adabu za kwenda haja.
• Kujitwaharisha baada ya kwenda haja

MBINU ZA KUFUNDISHIA.
• Kwa njia ya maelekezo na kumuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi umuhimu na faida ya usafi.
• Mwalimu awaelekeze wanafunzi kwa vitendo namna ya kupiga mswaki, kukoga, kuchana nywele, kufua, kupiga pasi, n. k.
• Mwalimu kila mara awakague wanafunzi kwa usafi na unadhifu wa mwili na nguo.
• Awafahamishe wanafunzi faida za usafi na hasara za uchafu.

VIFAA VYA KUFUNDISHIA.
• Nguo chafu na safi.
• Miswaki
• Sabuni
• Kitana
• Kikata kucha n. k.

LENGO.
Ajue kuwa usafi ni sehemu ya Uislamu.

Kutawadha:
MBINU ZA KUFUNDISHIA
• Mwalimu awaelekeze wanafunzi kutawadha kwa vitendo na awape wanafunzi mazoezi ya kutawadha mmoja mmoja mbele ya darasa.
• Aorodheshe ubaoni yale yanayotengua udhu na kuwataka wanafunzi wayarudie.

VIFAA VY KUTUMI.
• Ndoo ya maji
• Makopo
• Kata, n. k.

LENGO.
• Aweze kutawadha
• Aweze kutaja yanayotengua udhu

AKHLAQ:
MBINU ZA KUFUNDISHIA.
• Kwa njia ya maelekezo na kumuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi umuhimu na faida ya usafi.
• Mwalimu awaelekeze wanafunzi kwa vitendo namna ya kupiga mswaki, kukoga, kuchana nywele, kufua, kupiga pasi, n. k.
• Mwalimu kila mara awakague wanafunzi kwa usafi na unadhifu wa mwili na nguo.
• Awafahamishe wanafunzi faida za usafi na hasara za uchafu.

VIFAA VYA KUTUMIA.
• Nguo chafu na safi.
• Miswaki
• Sabuni
• Kitana
• Kikata kucha n. k.

LENGO
Ajue kuwa usafi ni sehemu ya Uislamu

ADABU ZA KULA:
MBINU ZA KUFUNDISHIA.
• Mwalimu awafahamishe wanafunzi vyakula vya halali akizingatia umri wao.
• Kwa njia ya maelekezo na kuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi vyakula vizuri vinavyokamilisha mlo na umuhimu wake katika mwili kulingana na umri wao.
• Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa vitendo namna ya kula kwa taratibu za Kiislamu.

VIFAA VYA KUTUMIA.
• Chakula
• Ndoo ya maji
• Ndoo tupu
• Glasi za maji, n.k.

LENGO.
Aweze kula kwa kuzingatia Sunnah

No comments:

Post a Comment