Monday, 30 January 2012

KUSOMA QUR-ANI (DARASA LA KWANZA:

Kusoma kwa ufasaha sura ya:-
• Al-Fatiha mpaka Al- A’laa
• Kuhifadhi sura hizo
• Kuandika
o Al-Fatiha
o Annas
o Al-Falaq
o Al-Ikhlas

• Mwalimu awasomee wanafunzi sura huku wakisikiliza kisha awaamuru kusoma katika kundi kisha mmoja mmoja.
• Mwalimu awawezeshe wanafunzi kuhifadhi kwa kumfuatisha bila kuangalia kitabuni kwa kundi na kisha mmoja mmoja.
• Mwalimu aandike ubaoni sura anayosomesha.
Mwalimu awaamuru wanafunzi kuandika al-Fatiha, annas, Al-Falaq na Ikhlas.

VIFAA VYA KUTUMIA.
• Ubao na chaki.
• Vibao vya wanafunzi.
• Radio kaseti.
• Kitabu cha I (IPC).

LENGO (MWANAFUNZI).
• Aweze kusoma Qur’an kwa ufasaha na kuhifadhi.
• Aweze kuandika Al-Fatiha, Annas, Alfalaq na al-Ikhlas.

No comments:

Post a Comment