NINI CHA KUFANYA ILI TUSOMESHE NA TUSOME HIZI ELIMU ZA KI-SECULAR, KWA MPANGO WA KIISLAMU??
1. Walimu Waislamu wa mashuleni wajitolee kuandika masomo ya shuleni bila kubadilisha syllabus kwa mpango wa kiislamu.
Kila Sura (chapter) iwe na utangulizi wa aya za Qur-ani na Hadithi kuhusu Sura hiyo, na ndani ya Sura hiyo pia, kuweko na aya ya Qur-ani na Hadithi.
Sura hizo pia zitoe mchango wa Waislamu kwenye somo hilo, bali kwenye kipengele hicho pia.
2. Kuwe na masomo ya dini kwa uhakika wa masomo hayo. Masomo hayo ni kama sheria ya Kiislamu, Sira, Tabia na mambo ambayo yanamuathiri Muislamu kila siku.
Isiwe kama shule zetu, tunamfundisha mtoto wetu jinsi ya kutoa hoja za dini, jinsi ya kujibizana na kafiri na asiye na dini lakini ukimwuliza jinsi ya kuswali, hajui, akienda chooni anajisafisha vipi, hajui. Wakati haya ndio masuala muhimu zaidi kuliko kujua kutoa hoja.
3. Walimu waambizane wenyewe kwa wenyewe umuhimu wa suala hili, walitangaze na kuliendeleza suala hili, na kila mmoja afanye kilicho kwenye uwezo wake.
Kila mtu afikishe ujumbe kwa mwenziwe, mwenye elimu atoe mchango wa elimu, mwenye pesa atoe mchango wa kuchapisha vitabu, mashule na kadhalika.
4. Ikiwa tutasubiri mpaka tuunde Chama, Kamati, Jumuiya ambayo itashughulikia suala hili, hatutafika popote. Tunajua udhaifu wetu, kila mmoja atakuja na makusudio yake, wengine watakuja ili wajaze mifuko yao na matumbo yao, wengine watakuja ili wapate umaarufu, na wengine watawekwa na vikundi ambavyo si vya Waislamu ili waharibu hiyo Jumuiya na mwisho tutavunja Jumuiya yetu.
Mwenyezi Mungu atupe uwezo wote, wa kuutumikia Uislamu na Waislamu kwa njia bora na ambayo anairidhia Yeye - Aamin.”
No comments:
Post a Comment